“Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Morogoro
tunapongeza ujasiri wa Rais Dk John Magufuli kusimamia na kuzindua mradi
wa Stiegler’s Gorge baada ya kucheleweshwa miaka mingi kukwamisha fursa
za kiuchumi na sasa Tanzania ikithibitisha kwa vitendo kuwa ni nchi
huru inayojiamulia mambo yake” Shaka
“CCM Mkoa Morogoro tunapongeza msimamo wa
Serikali ya Dk Magufuli kwani baada ya kukamilika mradi huo, utakaotoa
megawati 2,100 zitakazomaliza matatizo ya umeme na kusukuma mbele sekta
za uvuvi, kilimo na utalii na hatimae milango ya fursa za ajira kwa
vijana kufunguka” Shaka
“Stiegler’s Gorge ambao umekuwa ukipigwa
vita na danadana nyingi toka kwa matapeli waliozowea kujipatia fedha na
utajiri, utalipa heshima taifa kwa kujali na kusimamia maamuzi yake bila
kutikiswa ambapo tumeonyesha namna gani kama taifa lililo huru hatuko
tayari tena kukatishwa tamaa au kupangiwa, maendeleo, kupanga , kuchagua
na kuamua lipi na kufanya na lipi la kuacha kwa maslahi ya taifa na
watu wake” Shaka
“Mradi wa Stiegler’s Gorge utafungua
fursa zilizojificha mkoani morogoro na nchi yetu . Utatupa heshima ya
kusimamia mipango na maamuzi sahihi. Sis ni Taifa huru linalojali
maendeleo . Hatuna umasikini bali wapo watu wachache waliokosa shime na
ari ya uzalendo ” Shaka
“Nchi za kiafrika hazikupigania ukombozi
ili zijitawale na kupangiwa mambo yake, badala yake zina wajibu wa
kusimamia hatari ya umasikini kwa wananchi wake na kulinda heshima na
kuonyesha ziko huru” Shaka
“Tumesimamia uamuzi huu ili kulinda utu
na heshima ya kujitawala . Rais wetu kila kukicha anaumwa na umasikini
uliopo . amedhamiria, amesimamia sasa anatekeleza, hiii ni ndoto
iliosubiriwa miaka mingi na watanzania
baada ya kucheleweshwa kwa hakika kila mtanzania anayo kila sababu kusimama na Rais Magufuli ” Shaka
“Haiwezekani serikali ikahubiri mpango wa
maendeleo bila kuwa na mkakati wa sera unaoonyesha kufikisha nishati ya
umeme vijijini ambako ndiko kwenye mamilioni ya wakulima, wavivu na
wafugaji wanaokosa umeme” Shaka
“Serikali ya awamu ya tano itatunza
mazingira kwa kunusuru miti na misitu yetu isikatwe kuni na mkaa. Ili
kuzuia tusiteketeze miti tuwe na umeme wa uhakika .Hiyo ndiyo tiba ya
hakika .Umeme huchochea ujenzi wa viwanda kuelelea uchumi wa kati” Shaka
“Vijana kuweni na uzalendo na kulinda
mradi huu katika kila hatua sambamba na kutumia fursa ya mradi huu kama
chanzo kingine cha kuinua uchumi wa mtu moja moja kwa kufanya biashara
za uzalishaji kwa vile kuna mahitajio makubwa kipindi hiki cha ujenzi na
baada hivyo wanamorogoro waitumie vyema fursa hiyo” Shaka.
“Utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM
unakwenda kwa kasi sana hapa Morogoro vijijini CCM iliahidi mambo kadhaa
tunaendelea kuyatekeleza hatua kwa hatua hili ni moja wapo muelewe
wananchi baada ya kukamilika mradi huu mkubwa wa kimkakati fursa zaidi
za kiuchumi zitaongezeka ikiwemo kutunza mazingira, ujenzi wa viwanda,
uwekezaji na uanzishaji miradi ya kiuchumi mikubwa na midogo kazi kwetu
hususan vijana katika kutumia fursa hizi ” Shaka
0 comments:
Post a Comment