Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,
akisaini kitabu cha wageni katika kituo cha kuzalisha umeme, alipofanya
ziara ya kukagua utendaji kazi katika kituo hicho.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,(
katikati) akikagua mitambo ya kuzalisha umeme katika kituo cha kufua
umeme mkoani Kigoma.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,(
katikati) akiwapa maelekezo wasimamizi wa mitambo ya kufua umeme katika
kituo cha kuzalisha a umeme mkoani Kigoma.
Watendaji wa kituo cha kuzalisha umeme
cha Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nishati
Subira Mgalu.( katikati) , alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi
katika kituo hicho.
…………………….
Na Zuena Msuya Kigoma,
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
amesema Serikali inatarajia kuokoa takribani shilingi bilioni 25
zinazotumika kununua mafuta mazito ya kuendesha mitambo ya kuzalisha
umeme katika Mkoa wa Kigoma kwa mwaka.
Akizungumza baada ya kutembelea kituo cha
kuzalisha umeme mkoani Kigoma , Julai 12, Mgalu alisema serikali
itaokoa fedha hizo, baada ya kuunganisha mkoa huo katika gridi ya taifa
na kuacha kutumia umeme unaozalishwa kwa kutumia mafuta mazito.
Alisema kuwa tayari ujenzi njia ya
kusafirisha umeme kuunganisha Mkoa wa Kigoma katika gridi taifa umeanza
ambapo itapita katika Wilaya ya Urambo mkoani Tabora,Nguruka, na
Kidawe mkoani Kigoma.
Vilevile aliweka wazi kuwa tayari ujenzi wa vituo vya kupokea na kupoza umeme katika njia hiyo ya kusafirisha umeme umeanza.
“Serikali imekuwa ikitumia shilingi
bilioni 25, kila mwaka kununua mafuta mazito ya kuendesha mitambo ya
kuzalisha umeme Kigoma, lakini imekuwa ikiuuza umeme huo kwa shilingi
bilioni 10 tu, hii ni hasara, hivyo tunatekeleza mpango mathubiti wa
kumaliza changamoto hii”,alisema Mgalu.
Mradi huo ni wa kusafirisha umeme wa Kilovolti 132, na unatarajiwa kukamilika mwezi June 2020.
Akizungumzia hali ya upatikanaji wa umeme
katika mkoa huo,Mgalu alisema mkoa huo unahitaji umeme zaidi, ila kwa
sasa upo mpango wa kuongeza mitambo ya kufua umeme katika wilaya zenye
mahitaji makubwa zaidi ikiwemo Wilaya ya Kasulu.
Mitambo hiyo ni ile iliyozimwa katika
mikoa ambayo ilikuwa inatumia mafuta mazito kufua umeme , ambapo kwa
sasa tayari imeunganishwa katika gridi ya taifa, na kuacha kutumia umeme
unaozalishwa kwa kutumia mafuta mazito.
Sambasamba na hilo, alitoa wito kwa
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)kuwa, ujenzi wa njia ya umeme
ukikamilika uende sambasamba na uimarishaji wa upatikanaji wa huduma ya
umeme.
Pia kusitokee changamo ya kukatika kwa
umeme mara kwa mara kwa lengo la kuwapatia huduma bora watumiaji katika
kuendesha shughuli za uzalishaji.
“ Tanesco katika mradi huu
mjipange,mtimize azma ya serikali ya kuwapatia wananchi umeme wa kutosha
na wa uhakika,wananchi wajue kweli wameingia kwenye gridi, siyo
wanaingia kwenye gridi umeme unakatika hapana,nawapa tahadhari mapema,”
alisisitiza Mgalu.
Akiuzungumzia fursa za Mkoa wa Kigoma,
Mgalu amesema, serikali imedhamiria kuufanya Mkoa wa Kigoma kuwa wenye
viwanda na kuwavutia zaidi wawekezaji kwa kuwa mazingira yanaruhusu.
0 comments:
Post a Comment