Naibu Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza
na Mmiliki wa shule za Musabe zilizoko mkoani Mwanza Daniel Musabe
wakati wa oporesheni ya kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la
ardhi katika mkoa wa Mawanza mwishoni mwa wiki. Wa kwanza kulia ni Mkuu
wa Kitengo cha Kodi Wizarani Denis Masami na wa tatu kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi wa shule za Musabe Faustine Magabilo.
Naibu Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akihakiki
deni la kodi ya pango la ardhi la kampuni ya Birchard Oil Limited pamoja
na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Arshad Jetha (kushoto) wakati wa
oporesheni za kuwatembelea wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika
mkoa wa Mawanza mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi
Wizarani Denis Masami.
Kamishna
Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo (wa tatu kulia)
akifafanua jambo kwa Meneja wa Kampuni ya Ideal Development Ltd
Burnanuddin Rajbhai (wa kwanza kushoto) wakati Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipoitembelea kampuni
ya Ideal Development Limited katika operesheni ya kufuatiliawadaiwa
sugu wa kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Mwanza mwishoni mwa wiki.
Wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Dorothy Mwanyika na wa
pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizarani Denis Masami.
Naibu Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akihakiki
deni la kodi ya pango la ardhi la kampuni ya Jesse and Company Ltd
wakati wa oporesheni ya kufuatilia madeni ya kodi ya pango la ardhi
katika mkoa wa Mawanza mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi
wa Jesse and Company ltd Sundeep Bachu.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiagana na Afisa MfawidhiwaMaabara ya Taifa ya Udhibiti Samaki na Mazao ya UvuviEmanuel Mundoko wakati wa oporesheni ya kufuatilia madeni ya kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Mawanza mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimpa
maelekezo Meneja Rasilimali Watu wa kapmuni ya Synergy Tanzania Ltd ( wa
kwanza kulia) wakati wa oporesheni ya kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi
ya pango la ardhi katika mkoa wa Mawanza mwishoni mwa wiki. Wa kwanza
kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizarani Denis Masami. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).
………………………
Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA
Naibu Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amezidi kuzibana Taasisi na
Makampuni yenye madeni makubwa ya kodi ya pango la ardhi ambapo ametua
mkoani Mwanza na kuyabana makampuni na taasisi nane ambazo kwa ujumla
wake zinadaiwa zaidi ya milioni 900.
Kampuni na
taasisi alizotembelea Dkt Mabula ni Synergy Tanzania Ltd, Ideal
Development Ltd, Birchard Oil Ltd, Shule za Musabe, Taasisi ya Taifa ya
Utafiti Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Ndamavyo Auto Spares, Jesse &
Company Ltd na Maabara ya Taifa ya Udhibiti Samaki na Mazao ya Uvuvi.
Akizungumza
katika ziara yake hiyo ya kufuatilia madeni ya kodi ya pango la ardhi
mwishoni mwa wiki, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
alisema ziara hiyo anayoifanya ya kuwafikia wale wenye madeni makubwa
inafuatia baadhi ya kampuni na taasisi zinazodaiwa kushindwa kulipa ama
kurekebisha madeni yao baada ya kikao cha Juni 11, 2019
kilichowakutanisha wadaiwa zaidi ya 200 jijini Dodoma
katika mwanzo wa ziara yake kwenye shule za Musabe, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazialimueleza
mmiliki wa shule hizo Daniel Musabe kulipa deni lake la kodi ya pango
la ardhi linalofikia milioni 57.4 katika viwanja vyake vinne
anavyomiliki kufikia tarehe 31 Julai 2019 ili kuepuka kufikishwa katika
Baraza la Ardhi na Nyumba.
Hata hivyo,
Mmiliki wa Shule hizo ambazo ni za Chekechea, Msingi na Sekondari
alimueleza Dkt Mabula kuwa yuko tayari kulipa deni la kodi ya pango la
ardhi lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na changamoto za
kibiashara ambapo hata hivyo aliahidi kulipa kiasi anachodaiwa kuanzia
Agosti 2019 na kumaliza deni lote ifikapo Desemba 2019.
Akiwa katika
Kampuni ya Birchard Oil Limited, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula ambaye aliambatana na Mkuu wa Kitengo cha
Kodi Wizarani Denis Masami aliitaka kampuni hiyo kulipa kiasi
inachodaiwa cha kodi ya pango la ardhi inayofikia milioni 85,235,050
ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya kodi za miaka ya nyuma.
Meneja
uhusiano wa Kampuni hiyo inayojishughulisha na uzalishaji Mafuta na
Marobota ya Pamba Arshad Jetha alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi kuwa
kampuni yake pamoja na kudaiwa kodi ya pango la ardhi kwa baadhi ya
viwanja inavyomiliki lakini baadhi yake alishalipia hivyo aliomba
kuhakikiwa madeni yake ili kupata deni halisi.
Ideal
Development Ltd kupitia Meneja wake Burnanuddin Rajbhai alikiri deni la
kodi ya pango la ardhi linalofikia milioni 79 na kuomba kupewa muda wa
kulipa katika awamu tatu tofauti. Hata hivyo, Naibu Waziri wa Ardhi
alizitaka kampuni na Taasisi zilizokubali kulipa madenikuandika
barua ya kueleza namna zitakavyolipa na muda wa mwisho wa kulipa madeni
yao katika ofisi za ardhi za halmashauri husika na nakala za barua hizo
ziende ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi wa Kanda ya Ziwa.
Kamishna
Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo aliionya kampuni ya
Ideal Development Ltd kwa kushindwa kutekeleza makubaliano yaliyofikia
ya kulipa deni lake na kuieleza kuwa hatua itakayofuata kwa kampuni hiyo
ni kufikishwa katika Baraza la Ardhi na suala la kuingia makubaliano ya
malipo haliwezi kufanyika kwa mara ya pili.
Kampuni ya
Synergy Tanzania Ltd Kupitia kwa Meneja Utawala wake Florence Kivamba
iliahidi kuandika barua ya makubaliano ya kulipa deni la milioni 43
inayodaiwa ingawa alioamba kufanya mawasiliano na uongozi wa juu kwa
kuwa ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi ilikuwa ya kushtukiza na uongozi
haukuwepo.
Akiwa katika
Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Naibu Waziri wa
Ardhi Dkt Mabula aliueleza uongozi wa Taasisi hiyo kuwa inadaiwa jumla
ya shilingi milioni 515,713,900 ya kodi ya pango la ardhi na taasisi
hiyo haijawahi kulipa kodi hiyo tangu mwaka 1996.
Mkurugenzi
wa NIMR mkoa wa Mwanza Safari Kinuhi alijitetea kwa kueleza kuwa taasisi
yake inapaswa kusamehewa kulipa kodi ya pango la ardhi kwa kuwa haiko
kibiashara bali inatoa huduma kwa wananchi na kuboresha afya ingawa
aliahidi kuwasiliana na uongozi wa juu kuhusiana na suala hilo.
Hata hivyo,
Dkt Mabula alimueleza kuwa Taasisi yake inapaswa kufuata sheria wakati
wa kuomba kusamehewa kodi ya pango la ardhi huku Mkuu wa Kitengo cha
Kodi Wizarani Denis Masami akisisitiza kuwa hata kama Taasisi hiyo
itasamehewa kulipa kodi hiyo lakini deni la nyuma lazima lilipwe kwa
kuwa sheria ya msamaha itaanza pale tamko la msamaha lilipotoka.
Maabara ya
Taifa ya Udhibiti Samaki na Mazao ya Uvuvi iliyopo eneo la Nyegezi
ilionekana kutokuwa na hati ya eneo inalomiliki ingawa Afisa Mfawidhi wa
Taasisi hiyo Emanuel Mundoko alijitetea kwa kueleza kuwa awali Taasisi
hiyo ilikuwa sehemu ya chuo cha Uvuvi na sasa inajitegemea hivyo hawajui
madeni halisi wanayodaiwa.
0 comments:
Post a Comment