Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na Waoneshaji kwenye ufunguzi wa
Maonesho ya Utalii wa Utamaduni ya Serengeti yanayofanyika wilayani
Serengeti mkoani Mara. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Serengeti
Nurdin Babu akiwa na pamoja na viongozi wengine.
Naibu Waziri wa Malasili na Utalii,
Mhe.Constantine Kanyasu (wa kwanza kushoto) akiwa na Mbunge wa
Serengeti, Mhe.Chacha Ryoba ( katikati) wakipewa maelezo na muuza
vinyago ambaye ni miongoni mwa Washiriki wa Maonesho hayo ya Utalii wa
Kiutamaduni huku akiwa ameshika kinyago alipokuwa akimuelezea ubora wa
Kinyago hicho katika Maonesho ya Utalii wa Utamaduni ya Serengeti
yaliyofunguliwa rasmi mkoani Mara. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa
Maonesho hayo, Joshua Nyansiri.
Naibu Waziri wa Malasili na Utalii,
Mhe.Constantine Kanyasu akiwa na Mbunge wa Serengeti, Mhe.Chacha Ryoba
wakipewa maelezo kuhusu dawa za mitishamba kabla ya kuzindua Maonesho
ya Utalii wa Kiutamaduni ya Serengeti .
Naibu Waziri wa Malasili na Utalii,
Mhe.Constantine Kanyasu ( katikati) akiwa ameshika fimbo ikiwa ni zawadi
aliyokabidhiwa na Mkuu wa kikundi cha Utamaduni, Chacha Sengwa kama
ishara ya shukrani ya kukubali kufungua Maonesho ya Utalii wa Utamaduni
ya Serengeti mkoani Mara.Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Wa pili kulia ni
Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Mhe. Nurdin Babu
Naibu Waziri wa Malasili na Utalii, Mhe.Constantine
Kanyasu ( katikati) akikabidhiwa fimbo ikiwa ni zawadi aliyokabidhiwa
na Mkuu wa kikundi cha Utamaduni, Chacha Sengwa kama ishara ya shukrani
ya kukubali kufungua Maonesho ya Utalii wa Utamaduni ya Serengeti mkoani
Mara.Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya
Serengeti, Mhe. Nurdin Babu
Mku wa wilaya ya Serengeti, Mhe. Nurdin Babu akizungumza na
Waoneshaji kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Utalii wa Utamaduni ya
Serengeti yanayofanyika wilayani Serengeti mkoani Mara kabla ya
kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine
Kanyasu kwa ajili ya kufungua maonesho hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.
Constantine Kanyasu akiwa ameshika pambo ambalo imetengenzwa na
Mjasiliamali huku akipewa maelezo na Anna Chengula kabla ya kufungua
maonesho hayo.
( Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
………………
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.
Constantine Kanyasu ameiagiza Hifadhi za Taifa ( TANAPA) kupitia upya
sheria ya tozo ya kiingilio kwa watalii wanapotoka nje ya Hifadhi
inayowalazimu kulipwa tena wanapoingia ndani ya Hifadhi maarufu kwa jina
la Single Entry waiondoe kwenye maeneo yanayolalamikiwa kuwa imeua
shughuli za Utalii kwenye vijiji vinavyozunguka Hifadhi.
Aidha,Mhe. Kanyasu ameagiza TANAPA
iangalie maeneo ambayo inadhani ni muhimu kwa Single Entry iendelee
kutumika kuwa waweke mfumo wa kielektroniki wa utambuzi wa vidole (
Biometric Identity) utakaoweza kutumika kubaini udanganyifu endapo
utafanyika.
Amesema mfumo huo utawalazimisha watalii kuweka kidole wakati wakiwa wanaingia na wakati wanapotoka nje ya Hifadhi.
Amesema hali hiyo itawasaidia Waongoza
watalii kutoka nje ya Hifadhi na Watalii wao kwa ajili kuzitembelea
jamii zilizokaribu na Hifadhi na hivyo kuzisaidia jamii kunufaika moja
kwa moja kupitia utalii wa kiutamaduni.
Hayo yamesemwa kupitia Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakati alipokuwa akifunga
Maonesho ya 8 ya Utalii wa Utamaduni ya Serengeti mkoani Mara.
Amesema tangu kuanzishwa kwa Single Entry
kumepelekea madhara makubwa kwa baadhi ya maeneo yaliyo karibu na
Hifadhi za Taifa kudumaa kiutalii.
Ameyataja maeneo hayo yaliyokaribu na
yaliyoathirika moja kwa moja kuwa ni ukanda wa Magharibi katika geti la
Ndabaka katika Hifadhi ya Serengeti na katika Hifadhi ya Ruaha.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa Maonesho
hayo, Kanyasu amesema maeneo yaliyoathirika zaidi kutokana na kuwepo kwa
Single Entry ni yale maeneo ambayo hayajapitiwa na barabara kuu pamoja
na viwanja vya ndege.
Ametaja sababu zilizopelekea kufa
kiutalii maeneo hayo kuwa watalii walio wengi hulazimika kukaa ndani ya
Hifadhi hadi muda wa masaa 24 yanavyoisha bila kutoka wakikwepa
gharama endapo watatoka.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya
Serengeti, Nurdin Babu alimueleza Naibu Waziri huyo kuwa wilaya yake
asilimia 80 ni eneo la Hifadhi ya Taifa ya Serengeti hivyo kutokana na
uwepo wa Single entry wilaya hivyo imeathirika sana kwa vile imekosa
watalii wanaotembelea vijijini tofauti na ilivyokuwa mwanzo kabla ya
kuanzishwa.
” Mhe.Waziri tunakuomba uliangalie suala
hili, utalii wa kiutamaduni uliosaidia kuajiri wananchi wengi umekufa
kutokana na Single Entry” alisisitiza
Ameongeza kuwa endapo itaondolewa
itasaidia watalii kuweza kutoka nje ya Hifadhi kuembelea vituo vingi vya
utalii ambavyo vipo nje ya Hifadhi.
Naye, Anaeli Kilemi aliyesoma risala
mbele ya Waziri huyo amesema Single entry imewadidimiza wananchi wengi
ambao walikuwa wamejiajiri kupitia utalii wa kiutamaduni, Hivyo anaiomba
serikali itatue tatizo hilo.
0 comments:
Post a Comment