Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma,
Godwin Kunambi akizungumza na viongozi wa Shirika la Umoja wa Machinga
Tanzania walipomtembelea Ofisini kwake ambapo pia walimpatia cheti cha
shukrani kwa mchango wake kwa Machinga
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Umoja wa Machinga
Tanzania (SHIUMA) walipomtembelea ofisini kwake n kumkabidhi Cheti cha
Shukrani kwa kutambua mchango wake kwa machinga
………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
SHIRIKA la umoja wa Machinga Tanzania
limetakiwa kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Mafuguli kutaka Machinga wafanye shughuli zao pasipo
kusumbuliwa na mamlaka nyingine.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi alipokuwa akiongea na
kamati tendaji ya Shirika la Umoja wa Machinga Tanzania walipomtembelea
ofisini kwake kumkabidhi cheti cha shukrani leo.
Kunambi alisema “ndugu zangu, tunawajibu
wa kumsaidia mhe Rais kama wadau. Mhe Rais amefanya jitihada kubwa
katika kuhakikisha machinga wa nchi hii wanafanya shughuli zao katika
mazingira mazuri.
Tumeona utaratibu wake wa vitambulisho
vya wafanyabiashara wadogo. Vitambulisho hivi vimekuwa msaada mkubwa kwa
wafanyabiashara wadogo” alisema Kunambi.
Katika kuhakikisha Machinga wanafanya
kazi zao vizuri, Mkurugenzi huyo alisema kuwa Jiji la Dodoma linataka
kufanya Machinga wa kisasa. Machinga wanaofanya kazi zao vizuri kwa
kuzingatia taratibu.
Aidha, aliwataka kufanya shughuli zao na
kukua kimtaji. “Lazima tuwe na mpango wa kufanya mabadiliko kutoka
Machinga kwenda kuwa wafanyabiashara. Hata Mbuyu ulianza kama mchicha”
alisema Kunambi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirika la
Umoja wa Machinga Tanzania, Ernest Masanja alisema kuwa umoja huo
umeamua kumpatia cheti hicho kumshukuru Mkurugeni wa Jiji la Dodoma
kutokana na ushirikiano ambao amekuwa akiutoa kwa Machinga katika
kutekeleza majukumu yao.
Jiji la Dodoma ni miongoni mwa
Halmashauri ambazo zimemaliza kuuza vitambulisho vyote walivyopewa kwa
ajili ya kuwauzia wafanyabiashara wadogo.
Vitambulisho 15,173 vya wajasiliamali vimeshauzwa kwa wafanyabiashara kwa bei ya shilingi 20,000 kwa kila kimoja.
Rais John Magufuli aliamua kutoa
vitambulisho na kuagiza mamlaka zinazohusika kuwa vitambulisho hivyo ni
maalumu kwa wafanyabiashara ambao mtaji wao hauzidi Shilingi milioni nne
(4) ili viwasaidie kuzitambulisha biashara zao.
Aidha, aliagiza kuwa wafanyabiashara
watakaogawiwa vitambulisho hivyo wasisumbuliwe na mtu yeyote wakati wa
kufanya shughuli zao.
Lengo ni kuwafanya wafanyabiashara wadogo kutambuliwa rasmi na kutobughudhiwa wanapofanya biashara zao za halali
0 comments:
Post a Comment