Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akifuatilia mada
mbalimbali kwenye kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika
katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea
katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dkt.Bashiru Ally na kulia ni
Mkurugenzi Mkuu Takukuru, Diwani Athuman.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akifurahia jambo
katika kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika
Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika
viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Assad, Katibu Mkuu wa
Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dkt.Bashiru Ally.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),
Dkt.Bashiru Ally, akiteta Jambo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali Prof. Musa Assad, kwenye kongamano la siku maalum dhidi ya
Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara
Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius NyerereJijini Dar es
Salaam,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika akufuatilia
mijadala mbalimbali kwenye kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa
iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba
yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam,
kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Musa
Assad (wa kwanza kushoto), Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),
Dkt.Bashiru Ally.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa, Takukuru, Diwani Athuman akisisitiza jambo wakati
wa kuwasilisha Mada yake kuhusu Mwelekeo wa Taasisi hiyo katika
mapambano dhidi ya Rushwa, katika kongamano la siku maalum dhidi ya
Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara
Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es
Salaam.
Washiriki wa kongamano la siku maalum
dhidi ya Rushwa lililofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya
Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini
Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini kongamano hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa, Takukuru, Diwani Athuman akiwasilisha Mada mbele ya
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maanajimenti ya Utumishi na Utawala Bora,
Kapt.Mstaafu George Mkuchika, kuhusu Mwelekeo wa Taasisi hiyo katika
mapambano dhidi ya Rushwa, kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa
iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba
yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
huku kauli Mbiu yake ikiwa ni ‘Usindikazi wa Mazao ya Kilimo kwa Maendeleo Endelevu ya Viwanda’
(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)
…………………..
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
DAR ES SALAAM
WAZIRI wa nchi, Ofisi ya Rais
(Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), George Mkuchika
amesema Tanzania inaendelea kupata heshima kubwa katika Jumuiya ya
Kimataifa katika vita vya mapambano dhidi ya rushwa kutokana na
mshikamano na nguvu ya pamoja iliyopo katika vyombo na taasisi
zinazosimamia utawala bora nchini.
Akizungumza katika kongamano la siku
maalum dhidi ya rushwa katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara
yanayoendelea Jijini Dar es Salaam leo Jumatano (Julai 3, 2019) Waziri
Mkuchika alisema utafiti uliofanywa na taasisi hizo zimesifu juhudi za
zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano na kuitaja Tanzania kuwa ni
nchi ya mfano katika vita vya mapambano dhidi ya rushwa.
Mkuchika aliasema taasisi hizo zikiwemo
MO Ibrahim, Transparency International, APRM na taasisi nyingine kubwa
duniani zinazosimamia masuala ya utawala bora zimefanya utafiti na
kusifu juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya Tanzania chini ya Rais
Dkt. John Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa ambapo tafiti
mbalimbali zimeifanya Tanzania kushika nafasi ya pili nyuma ya nchi ya
Rwanda.
Waziri Mkuchika alisema Serikali ya Awamu
ya tano imeendelea kuweka mkazo na msukumo katika mapambano dhidi ya
rushwa ambapo taasisi zote zinazosimamia masuala ya utawala bora
zimekuwa zikiunganisha nguvu ya pamoja na kulifanya suala la rushwa sasa
kuwa na nguvu na msukumo mpya wa mapambano katika jamii.
“Kwa sasa vyombo vyetu vyote serikalini
si TAKUKURU pekee bali pia polisi, tiss (usalama wa taifa), Ofisi ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ICAG) na vingine vyote,
vimeendelea kuunga katika kusimamia masuala ya utawala bora na hili
limeleta msukumo na hamasa mpya katika vita dhidi ya rushwa hapa nchini”
alisema Waziri Mkuchika
Akizungumzia rushwa katika sekta ya
viwanda na biashara, Waziri Mkuchika alisema Serikali imeendelea kuweka
mikakati mbalimbali katika kupunguza tatizo hilo ambalo limekuwa
likiathiri sekta binafsi ambayo imekuwa mshirika wa karibu wa serikali
katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuchika alisema
rushwa katika sekta biashara imekuwa ikiathiri sana masuala ya uwekezaji
wa kigeni, ambapo eneo lililonyesha kutawala kwa rushwa ni katika eneo
la utoaji wa vibali na leseni kutoka katika taasisi na idara muhimu za
serikalini na hivyo serikali imeendelea kulifanyia kazi ili kuhakikisha
kuwa vikwazo hivyo vinaondolewa kwa wawekezaji na hivyo kuharakisha
ukuaji wa uchumi.
Akifafanua zaidi Mkuchika anasema
kutokana na serikali kutambua mchango wa sekta ya viwanda na biashara
katika kukuza uchumi na uzalishaji wa ajira nchini ili kufikia uchumi wa
kati ifikapo mwaka 2025, Serikali imekuwa ikifanya marekebisho
mbalimbali ya sheria na sera mbalimbali ambazo zimekuwa ni sehemu ya
mianya ya rushwa nchini ikiwemo eneo la kodi.
“Kutokana na kudhibiti rushwa kwa sasa
kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya mwezi yameweza kuongezeka kutoka Tsh
Bilioni 800 kwa mwezi hadi kufikia Tsh trilioni 1.3 hii inaoyesha kuwa
kulikuwa na maeneo ambayo kulikuwa na uvujaji wa mapato ya serikali
kulikochangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo rushwa”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Diwani Athumani
alisema serikali imeendelea kushirikiana na wadau wa sekta binafsi
kupitia Mpango Mkakati dhidi ya mapambano ya rushwa (NASCAP III) ili
kuhakikisha kuwa mapambano na vita dhidi ya rushwa yanapata mafanikio
nchini.
Anaongeza kuwa kupitia NASCAP III, ofisi
yake imeendelea kutekeleza masuala mbalimbaliu ikiwemo kufanya tafiti
kubaini ukubwa na kiwango cha rushwa nchini, kupokea maoni, kutoa elimu
kwa umma kupitia makongamano, rushwa pamoja na kufanya uchunguzi na
kufungua mashtaka kwa watu mbalimbali wanaopatikana na hatia dhidi ya
rushwa.
0 comments:
Post a Comment