Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akifundisha somo la Hesabu kwa wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Iyula wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo katika Jimbo la Vwawa leo tarehe 23 Julai 2019, (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza ulazima wa wanafunzi kusoma kwa bidii wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Iyula akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo katika Jimbo la Vwawa leo tarehe 23 Julai 2019.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika shule ya msingi Iyula wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo katika Jimbo la Vwawa leo tarehe 23 Julai 2019. Mwingine Pichani ni Mwalimu Mkuu wa shule huyo Ndg Barnaba Mahembe.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Iyula wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo katika Jimbo la Vwawa leo tarehe 23 Julai 2019
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Iyula wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo katika Jimbo la Vwawa leo tarehe 23 Julai 2019
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Mbunge wa Jimbo la Vwawa
Mkoani Songwe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameanza
ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo katika Jimbo la Vwawa.
Akiwa katika kata ya Iyula
Mhe Hasunga amekagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na kuzungumza na wanafunzi
wa shule ya msingi Iyula ambapo pamoja na mambo mengine amewasisitiza wanafunzi
hao kusoma kwa bidii ili kujikwamua katika wimbi la ujinga kadhalika kiuchumi.
Waziri Hasunga amewapongeza
walimu wa shule hiyo kwa mshikamano na usimamizi madhubuti wa fedha za ujenzi
wa vyumba hivyo viwili vya madarasa ambavyo vimefikia katika hatua nzuri ya
kuanza kutumika.
“Mna bahati sana kusoma
katika shule ambayo imetoa waziri wa kilimo hivyo ili kuwa na viongozi wengi
katika Taifa hili mnapaswa kusoma kwa bidii na kuongeza ufaulu katika Takwimu
za mkoa wetu” Alisema Mhe Hasunga
Pamoja na kuchangia shughuli
za maendeleo katika jimbo hilo la Vwawa lakini pia amewataka wanafunzi hao
kutambua kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe
Magufuli imejipanga kuimarisha elimu na imeanza na utoaji wa elimu bure kuanzia
ngazi ya awali mpaka sekondari.
Alisema kuwa lengo la Rais
Magufuli kuruhusu elimu kuwa bure ni kutaka kurahisisha upatikanaji wa elimu
kwa urahisi kwa wanafunzi wote nchini ili hata wale waliokosa fursa kutokana na
kipato duni cha wazazi waweze kuelimika na kuwa msaada katika familia zao na
Taifa kwa ujumla.
Mhe Hasunga amesema kuwa
pamoja na vitabu kuwasaidia wanafunzi kuelimika lakini wazazi na walimu ni
sehemu ya uimara wa mafanikio ya wanafunzi katika ufaulu wao.
“Mimi nawapongeza sana ninyi
wanafunzi kwani mna bahati kubwa kusoma katika kata zenu mnazoishi maana sisi
wakati tunasoma tulikuwa tukienda umbali mrefu kutafuta elimu jambo ambalo
lilikuwa likitukatisha tamaa ya kusoma” Alikaririwa Mhe hasunga
Mbunge wa Jimbo la Vwawa
Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga atakuwa na ziara ya
siku tano katika jimbo hilo ambapo pamoja na mambo mengine atashirikiana na
wananchi katika shughuli za maendeleo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment