
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na
wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Nyaseke
kuhusiana na umuhimu wa viongozi pamoja na wazazi katika kushirikiana
kwenye vita dhidi ya wanaume wanawapa mimba watoto wa kike wakiwa bado
shule.

Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ( wa pili
kulia)( akiwa na baadhi ya viongozi wa CCM wa wilaya ya Geita pamoja na
madiwani wa Kata ya Bulela na Shiloleli mara baada ya kuanza mkutano wa
hadhara ambapo pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kuwaeleza
wananchi wake ahadi mbalimbali alizozitekeleza yakiwemo masuala ya afya,
miundombinu pamoja mikopo tangu walimpomchagua kuwa Mbunge wao

Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Geita,
Barnabas Mapande akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara
akiwaeleza ahadi mbalimbali alizozitekeleza na anazoendelea kutekeleza
Mbunge wa Geita mjini, Mhe, Constantine Kanyasu

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Geita mjini, Mhe.Kanyasu wakati wa mkutano wa hadhara katika eneo la Bulela

Diwani wa viti maalum wa Bulela, Mhe,
Salome Kitula akizungumza na wananchi wa kata ya Bulela kabla ya
kumkaribisha Mbunge wa Geita mjini Mhe, Kanyasu kuzungumza na
wananchi.wa kata hiyo

Diwani wa viti maalum wa Kasamwa, Mhe.
Jesca Kalalio akizungumza na wananchi wa kata ya Kasemwa kabla ya
kumkaribisha Mbunge wa Geita mjini Mhe, Kanyasu kuzungumza na
wananchi.wa kata ya Bulela
………………….
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema
atawashughulikia Watendaji Kata wote watakaobainika kushindwa kuchukua
hatua kwa Wanaume wanaowapa mimba wanafunzi wa kike wakiwa bado shule.
Pia, Ametangaza vita kwa Waendesha
pikipiki (Bodaboda ) kuwa yeyote atakayebainika kumpatia mimba mtoto wa
kike akiwa bado shule hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Nyaseke Kata ya Bulela mkoani Geita.
Amesema mtoto wa kike anayepata mimba
akiwa shule na hivyo kulazimika kukatisha masomo yake haiwezi kuwa Mama
bora kwa sababu atashindwa tu kumlea watoto wake ipasavyo.
“Ninyi wanafunzi someni hata ukipata
daraja la mwisho baada ya kufika kidato cha nne ni lazima utakuwa Mama
bora” alisisitiza Kanyasu
Amesema maisha ya sasa yamebadilika sana tofauti na zamani ambapo kwa sasa bila kusoma maisha ni magumu sana
Mhe.Kanyasu amesema haiwezekani Serikali
itoe pesa nyingi kila mwezi katika shule zote nchini ili watoto wa kike
waweze kusoma huku idadi ya watoto wakike wanaoacha shule kwa sababu
za kupata mimba ikizidi kuongezeka.
” Nawambieni Watendaji wa Kata mkishindwa
kuwachukulia hatua waharibifu wa ndoto za watoto wa kike nitaanza na
ninyi” alisema Mhe.Kanyasu.
Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu
amewaonya wazazi wanaowalinda Wanaume wanaowapa mimba watoto wa kike
kwa kukubaliana nao kuwa ni jambo lisilokubalika.
” Mimi Mbunge wenu nimekuwa nikihakikisha
napigania ujenzi wa shule bora pamoja na walimu bora lakini baadhi ya
wazazi mmekuwa mkiwalinda wanaofanya uharibifu, si jambo zuri”
Amewataka wazazi waache tabia ya
kuelewana katika ngazi ya kifamilia kwa wanaume wanaokatiza ndoto za
watoto wa kike wakiwa bado shule.
” Nawasihi wazazi mzungumze na Watoto wa
kike kuhusu umuhimu wa kusubili huku mkiwasisitiza kuhusu umuhimu wa
elimu katika dunia ya sasa” amesititiza Mhe.Kanyasu.
Naye, Diwani wa viti maalum wa Kata ya
Bulela, Mhe, Salome Kitula amesema tatizo la mimba kwa watoto wa shule
ni kubwa linahitaji ushirikiano kwa wapenda maendeleo wote.
Amesema jitihada nyingi zimekuwa
zikifanyika ikiwa pamoja na kufanya semina na wazazi kuhusu umuhimu wa
kuwafuatilia watoto wakike wakiwa eansonesha mienendo isiyofaa pamoja na
kufanya ziara katika shule kwa ajili ya kuzungumza na wanafunzi kuhusu
athari za kupata mimba wakiwa bado shule.
Ameongeza kuwa kwa mwaka 2018 takribani wanafunzi zaidi ya kumi walibainika kupata mimba na tayari kesi zinaendelea mahakamani.
0 comments:
Post a Comment