Mbunge wa vijana Taifa ambaye pia ni
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Nishati na Madini Mh Mariam
Ditopile kwa niaba ya vijana amemshukuru Rais Magufuli kwa uzinduzi wa
mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji Mkoani Pwani kupitia
bwawa la kwanza kwa ukubwa Afrika Mashariki na kati, utakaogharimu kiasi
cha Shilingi Trilioni 6.5.
Mradi huo unategemewa kukamilika mwezi
June 2022 utazalisha megawati 2115 na unatajwa kuwa mwarobaini wa umeme
jambo ambao litachochea ukuaji wa Tanzania ya viwanda.
” Nina imani sasa ile ahadi ya Tanzania
ya viwanda kupitia chanzo hiki cha uhakika na cha gharama nafuu cha
Umeme inaenda kutimia rasmi sanjari na uhakika wa umeme wa kutosha ktk
mradi mkubwa wa treni ya mwendo kasi (SGR).
Sisi kama vijana hatuna budi kuishukuru
serikali yetu sikivu chini ya Rais wetu kipenzi Dk Magufuli na wasaidizi
wake wote kwa kuisimamia vyema na kwa dhati kabisa miradi hii, kwani
vijana ndio tunaenda kuwa wanufaika wakubwa,” amesema Mhe Ditopile.
Amesema kupitia miradi hii kuna ajira za
kudumu na ajira za vipindi maalum zitazaliwa jambo ambalo litapunguza
wimbi kubwa la vijana ambao hawana ajira.
” Kupitia miradi hii kuna fursa mbalimbali za kibiashara kwa mfano, mahoteli, migahawa, mama lishe, vifaa mbalimbali vya ujenzi.
Pia itakapokamilika miradi hii kwa upande
wa wafanyabiashara na watanzania kwa ujumla tutakuwa na umeme wa
uhakika na kushuhudia ndoto ya Rais Magufuli kuifikisha Tanzania katika
uchumi wa kati kupitia viwanda.
Mhe Ditopile amesema kwa upande wa
wakulima kupitia treni ya umeme utakaotokana na mradi huo wa Stiglera
Gorge watakuwa na uhakika wa kupata soko lenye tija.
” Kwenye hili tunamuahidi kwa dhati
kabisa Rais wetu tupo nae bega kwa bega kwa kuwa Watanzania wa leo
wanataka kazi na serikali yetu chini ya Rais Magufuli sasa ipo kazini,”
amesema Mhe Ditopile.
0 comments:
Post a Comment