Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza
na Viongozi, Watumishi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na wakazi wa
Marangu wakati wa hafla fupi ya kuwaaga vijana watakaopanda Mlima
Kilimanjaro ikiwa ni ishara ya kumbukizi ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa
Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi
Warioba akielezea jambo kwa vijana 8 walioshiriki katika shughuli hiyo
ya kupanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kuadhimisha kumbukizi ya miaka 20
ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Bi. Mwanaidi Ali.
Baadhi ya Watumishi wa Hifadhi ya Taifa
ya Mlima Kilimanjaro wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani) wakati wa
hafla ya kuwaaga vijana hao.
Sehemu ya Vijana wanaotarajiwa kupanda
Mlima Kilimanjaro kwa awamu ya pili wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (hayupo
pichani) kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima huo, Julai 26, 2019.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akimkabidhi Bendera ya Taifa
Kiongozi wa msafara huo Bw. Agustine Gusha mara baada ya kumalizika kwa
hafla hiyo iliyofanyika Mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (wenye kofia ya Bluu)
akiwasindikiza vijana hao kuashiria kuanza kwa safari yao ya kupanda
Mlima huo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akiwaaga Vijana hao nane (8)
kutoka Mkoa wa Songwe, Arusha, Tanga, Kaskazini Unguja na Kusini Unguja
alipowasindikiza vijana hao waliokuwa wakipanda Mlima huo. Kulia ni Mkuu
wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kippi Warioba.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro kwa ajili
ya kuwaaga vijana kutoka Mkoa wa Songwe, Arusha, Tanga, Kaskazini
Unguja na Kusini Unguja kabla ya kupanda Mlima huo.
Kamishna Mwandamizi wa Kanda ya
Kaskazini, Herman Batiho akimfafanulia Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (kulia) kuhusi hifadhi
ya Mlima Kilimanjaro, alipowasilia Mkoani huo kwa lengo la kuwaaga
vijana hao.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw.
James Kajugusi akielezea kuhusu vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro
kwa awamu ya pili ikiwa ni ishara ya kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha
Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (kulia) akijadili jambo na
Kamishna Mwandamizi wa Kanda ya Kaskazini, Herman Batiho alipowasili
katika hifadhi hiyo kwa lengo la kuwa kuwaaga vijana waliopanda Mlima
Kilimanjaro kwa awamu ya pili.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (katikati) akiwa kwenye picha ya
pamoja na Viongozi na vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro,
alipowasilia Mkoani huo kwa lengo la kuwaaga vijana hao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Mhe. Anna Mghirwa alipomtembelea ofisini kwake kabla ya
kuelekea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
………………….
Na; Mwandishi Wetu
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (Mb) amewataka
vijana kuenzi mchango wa Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere
kwa kuwa wazalendo na wenye mshikamano katika kujenga Taifa.
Mhe. Mavunde amesema hayo wakati wa hafla
fupi ya kuwaaga vijana kutoka Mkoa wa Songwe, Arusha, Tanga, Kaskazini
Unguja na Kusini Unguja kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni
ishara ya kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Nyerere
iliyofanyika Mkoani Kilimanjaro katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima
Kilimanjaro (KINAPA).
Alisema kuwa vijana wanapaswa kuwa
wazalendo kwa kuiga kivitendo yale yote yaliyotendwa na waasisi wa taifa
hili, Mwl. Julius K. Nyerere na Hayati Mzee Abeid Karume kwa kuendelea
kudumisha upendo, amani na mshikamo kwa mustakabali wa Taifa.
“Vijana waliowengi kipindi hiki wameweka
pembeni uzalendo wa kulipenda taifa lao hali ambayo inatubidi
tujitahmini na kuenzi falsafa walizokuwa nazo waasisi wetu ambao
waliweka maslahi ya Taifa mbele wakati wote,” alisema Mavunde
Akitolea mfano wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, namna ambavyo
amekuwa mstari wa mbele katika kuwatumikia wananchi kwa kutekeleza
masuala mbalimbali ya kitaifa wakati wote ili nchi isonge mbele
kimaendeleo.
Pia alitumia nafasi hiyo kuwapongeza
vijana waliopanda mlima huo awamu ya kwanza na awamu hii ya pili kwa
kuonesha ushujaa na uzalendo kwa Taifa lao ikiwemo kuwa mabalozi wazuri
katika kutangaza sekta ya utalii.
Aidha, Naibu Waziri Mavunde alitoa wito
kwa vijana kuacha kukaa kwenye vijiwe na kujihusisha kwenye mambo yasio
na tija, bali wajishughulishe kwenye miradi mbalimbali itakayo wawezesha
kiuchumi na kusaidia kukua kimaendeleo, kwa kuwa waasisi wa taifa
walikuwa wachapakazi, waadilifu na wabunifu ambao ni mfano mzuri wa
kuigwa.
“Hakuna nchi yoyote dunia ambayo inaweza
kuendelea pasipo kuhusisha nguvu kubwa ya vijana katika maendeleo ya
taifa,” alieleza Mavunde
Aliongeza kuwa ili kufikia malengo kwenye uchumi wa viwanda ni lazima vijana wazingatie uzalendo, utaifa na bidii katika kazi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Moshi,
Mhe. Kippi Warioba alisema kuwa kitendo cha vijana hao kushiriki katika
kupanda Mlima huo ni jambo muhimu kwa taifa na inaashiria namna gani
vijana wameanza kutambua historia ya waasisi wa taifa lao.
Naye, Kiongozi wa Vijana hao waliopanda
Mlima Kilimanjaro Bw. Augustine Gusha aliunga mkono maelezo yaliyotolewa
na Naibu Waziri na alitumia nafasi hiyo kuwasihi vijana kudumisha amani
ya nchi wakati wote.
Katika Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka
2019, Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana
inaratibu shughuli ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa Vijana 100 kwa ajili
ya kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere. Awamu ya kwanza vijana walipanda mlima huo tarehe 26
Machi, 2019 na awamu ya pili 26 Julai, 2019. Awamu ya Tatu itakuwa mwezi
Oktoba.
0 comments:
Post a Comment