Na Mwandishi wetu – Mwanza
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda,
amewataka wabunge na Mdiwani wa vitimaalum nchini kusimamia kikamilifu
rasilimali za umma ili ziwanufaishe wananchi wote.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, akitoa ufafanuzi wa jambo katika semina ya kujenga uwezo viongozi wanawake wa serikali za Mitaa (WASEMI).
Akizungumza
Jijini Mwanza katika semina ya kujenga uwezo kwa viongozi wanawake wa
serikali za Mitaa (WASEMI) iliyoandaliwa na shirika la TGNP Mtandao,
Makinda alisema kwamba, mchango wa wabunge na madiwani wa viti maalum
umekuwa hauonekani vizuri au kutambuliwa na jamii kutokana na wao
wenyewe kuwa na hofu au kutokujiamini kitu ambacho kimechangia
kuwarudisha nyuma na kushindwa kuendelea mbele.
“tatizo
letu sisi viongozi Wanawake, tunajenga hofu, tunaogopa sana kujitokeza
na kuwajibika vizuri kwa wananchi, eti kwa sababu ni viti maalum. Sisi
tulianzia pia viti maalum , lakini tulipata nafasi ya kwenda jimboni
kwasababu tulijiamini, tuliwajibika kikamilifu na tulihangakikisha uwezo
wetu unaonekana na kila mmoja. Jitokeze, kwa wananchi, watumikie kwa
uadilifu na watakuona na kutambua mchango wako” alisema Makinda
Makinda
amewaasa wanawake viongozi wa serikali za Mitaa, kuhakikisha
wanasimamia ubora wa huduma za jamii kwenye halmashauri zao na
kuhakikisha kila kinachofanyika kwenye halmashauri wanakielewa vizuri na
kutoa taarifa kwa wananchi wote.
Awali
akizungumza Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake viongozi wa serikali za
Mitaa (WASEMI), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya
Morogoro Bi. Kibena Kingo, alisema kwamba WASEMI itahakikisha wenyeviti
wa halmshauri wanawake wanaonesha mfano bora wa utendaji uliotukuka
kwenye halmashauri zao hasa kutokomeza rushwa, ubadhirifu wa mali za
umma na kuhakikisha kila senti iliyopangwa kwajaili ya kuboresha maisha
ya wananchi inatumika vizuri.
“Niwaombe
ndugu zangu, viongozi wanawake wa halmshauri pamoja na madiwani, sisi
wanawake tumeaiminiwa tukapewa nafasi, tusimamie vizuri rasilimali za
halmshauri zetu, tujenga mtandao wa kutokomeza Ukatili wa Kijinsia,
tutenge bajeti nzuri inayozingatia usawa wa kijinsia na kuboresha maisha
ya wananchi wote bila ubaguzi” alisema Bi. Kingo
Mkutano
huu ambao umeandaliwa kwa ushirikiano wa TGNP Mtandao na WASEMI
ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Serikali za Mitaa ALAT
Gulamhafeez Mukadam, na Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Bi.
Anjelina Mabula ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela jijini Mwanza.
Tanzani
ina Halmshauri 185, ambapo kati ya hizo, wanawake wanaoongoza
Halmshauri ni watano pekee ambazo ni halmashauri za Biharamulo, Hai,
Mwanga, Morogoro na Gairo. Ambao wamekubaliana kuhakikisha wanaweka
hitoria ya kuwa halmashauri za mfano kwa maendeleo na zenye kuzingatia
usawa wa kijinsia katika Nyanja za uongozi na mipango.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Serikali za Mitaa ALAT Gulamhafeez Mukadamika akitoa neno
katika semina iliyofanyika jijini Mwanza ya kuwajengea uwezo viongozi
wanawake wa serikali za mitaa.
Naibu
waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Bi. Anjelina Mabula ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Ilemela jijini Mwanza akiongea na washiriki wa semina
hiyo.
0 comments:
Post a Comment