Mkuu wa wilaya ya Mbozi Bw. John Palingo akipewa maelezo na Meneja wa RUWASA Mbozi Mhandisi Stephen Mkalimoto-Sengayave akikagua tanki la maji la Itaka lililokarabatiwa hivi karibuni.
Kaimu mkurugenzi Mtendaji Mbozi Bi Halima Mpita akionyesha uso wenye tabasamu baada ya kushuhudia kasi ya ujenzi wa mradi wa maji Itaka unaolenga” kumtua mama ndoo kichwani” kwa vijiji vitano vya kata za Bara, Itaka na Halungu.
Timu ya wataalamu wa Halmashauri wakiwa pamoja na Katibu Tawala wilaya ya Mbozi Bi Tusubileghe Benjamin (aliyepo katikati) wakipewa maelezo na Mkandarasi wa mradi huo Bw. Hezron Mwakyembe (kushoto) kwenye eneo la Chanzo cha Maji kinachojengwa Itaka.
Watoto wakiwa kwenye chanzo
hcho kuchota maji, mradi huu utakapokamilika utapunguza muda wa kusafiri
hadi kwenye chanzo kuchota maji na badala yake watachota ndani ya mita
400 kutoka kwenye makazi yao.
0 comments:
Post a Comment