METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, July 2, 2019

MATUKIO KATIKA PICHA: MAONESHO YA 43 YA BIASHARA SABASABA

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Kuhusu Maonesho ya 43 ya Biashara (sabasaba) ambayo yalianza Juni 28, 2019 na yatazinduliwa Rasmi Hapo Kesho na Makamu wa Rais wa Tanzania, Suluhu Hassan, huku kauli mbiu ikiwa ni “ Usindikaji wa mazoa ya kilimo kwa maendeleo endelevu ya Viwanda”.Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, Akiwa kwenye viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam, Tayari kwa kuanza kutembelea mabanda yaliyoko kwenye maonesho ya 43 ya biashara(sabasaba), Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bwana Edwin Rutegaruka
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa akiwa katika banda la kampuni ya kutengeneza Majani ya Chai (Chai Bora) alipokua akitembelea mabanda yaliyoko kwenye maonesho ya 43 ya biashara(sabasaba), wa pili Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bwana Edwin Rutegaruka.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, akipokea Maelezo kutoka kwa mjasiriamali wa asali ya asili katika maonesho ya 43 ya biashara(sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Maneja Msaidizi, Idara ya Uhusiano na Itifaki kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Vicky Msina, kuhusu historia ya Sarafu ya Tanzania, mara baada ya kutembelea katika Banda hilo, kwenye maonesho ya 43 ya biashara(sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar es Salaam, Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bwana Edwin Rutegaruka.
Elizabeth Daudi kutoka Dodoma Akionesha vitu vya asili katika kabila la Wagogo katika Maenesho ya 43 ya Biashara (sabasaba) ambayo yalianza Juni 28, 2019 na yatazinduliwa Rasmi Hapo Kesho na Makamu wa Rais wa Tanzania, Suluhu Hassan, huku kauli mbiu yake ikiwa “ Usindikaji wa Mazoa ya Kilimo kwa Maendeleo Endelevu ya Viwanda”.
 Afisa Habari kutoka kituo cha Uwekezaji, Latifa Kigoda, akielezea huduma ambazo Taasisi hiyo inazitoa kwa wawekezaji katika Maonesho ya 43 ya Biashara (sabasaba) ambayo yalianza Juni 28, 2019 na yatazinduliwa Rasmi Hapo Kesho na Makamu wa Rais wa Tanzania, Suluhu Hassan, huku kauli mbiu yake ikiwa “ Usindikaji wa Mazoa ya Kilimo kwa Maendeleo Endelevu ya Viwanda”.
 Moja ya Bidhaa kutoka katika kampuni ya kuunganisha Matrecta ya URSUS kama linavyonekana kwenye picha katika maenesho ya 43 ya Biashara (sabasaba) ambayo yalianza Juni 28, 2019 na yatazinduliwa Rasmi Hapo Kesho na Makamu wa Rais wa Tanzania, Suluhu Hassan, huku kauli mbiu yake ikiwa “ Usindikaji wa Mazoa ya Kilimo kwa Maendeleo Endelevu ya Viwanda”.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com