WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo amewataka wazazi
kutowasumbua watoto wao kwa kuwahamisha shule za serikali na kuwapeleka
shule binafsi.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jijini Dodoma waziri Jafo amesema kuwa shule za serikali
zimefanya vizuri ikilinganishwa na ufaulu wa hapo nyuma ambapo kila mtu
alizibeza
Waziri Jafo amebanisha siri ya shule
za serikali kufanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka 2019
kuwa ni kutokana na uwekezaji uliofanywa kwenye sekta ya elimu .
Hivyo Uwekezaji huo umepelekea ufaulu
kupanda kutoka asilimia 98.2 hadi 98.93,shule nne za serikali kuingia
katika kumi bora ya kwanza na katika shule 100 bora mwaka huu shule 64
ni za serikali ambazo 52 ni za kata na 12 ni shule kongwe na vipaji
maalum.
Mhe.Jafo ametaja shule nne zilizoingia 10 bora kuwa ni Kisimiri, Mwandeti, Tabora boys na Kibaha.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo
ameipongeza mikoa mitatu ambayo ni Arusha, Tabora na Pwani ambazo shule
za serikali zimefanya vizuri kwa kuingia 10 bora.
Hata hivyo,Waziri Jafo ameagiza
kufanyika tathmini kwa mkoa wa Mara ambao takribani shule 3 zipo kwenye
kundi la shule zilizofanya vibaya katika matokeo hayo.
0 comments:
Post a Comment