Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungmza
kwenye mkutano kati ya wananchi na Mbunge kuhusu ahadi mbalimbali
alizozitekeleza ikiwemo suala la utoaji mikopo wa shilingi bilioni 1.6
kwa vikundi mbalimbali wakiwemo vijana, wanawake na walemavu kwa lengo
la kupunguza umasikini katika jamii kwenye mkutano uliofanyika katika
kata ya Ihanamiro wilaya ya Geita mkoani Geita
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (katikati) akiwa
na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Geita, Mhe.Mohamed Ali( wa pili
kulia) pamoja na Diwani wa kata ya Ihanamiro, Joseph Lugaila wakiwa
kwenye mkutano wa hadhara kabla Mhe. Kanyasu kuanza kuzungumza na
wananchi wake katika kata ya Ihanamiro.
Baadhi ya wanachama wa CCM waliohudhuria
mkuatano wa Mbunge wa Geita mjini, Mhe. Constantine Kanyasu
wakimsikiliza wakatik akizungumza kwenye mkutano huo kuhusu ahadi
alizozitekeleza kwa wananchi wake likiwemo suala la mikopo kwa wanawake,
vijana na walemavu.
Baadhi ya Madiwani wa viti maalum
walioshirki kwenye mkutano wa Mbunge wa Geita mjini, Mhe. Constantine
Kanyasu wakimsikiliza wakati akizungumza na wananchi wake katika kata ya
Ihanamiro.
Baadhi ya wananchi walioshiriki kwenye
mkutano wa Mbunge wa Geita mjini, Mhe. Constantine Kanyasu wakimsikiliza
Mbunge wao wakati alipokuwa akizungyumza nao katika kata ya Ihanamiro.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita,
Mohamed Ali akizungumza na wananchi wa kata ya Ihanamiro kabla ya
kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na utalii ambaye pia ni Mbunge wa
Geita mjini kabla ya kuzungumza na wananchi wa kata hiyo.
Mbunge wa Geita mjini, Mhe. Constantine
Kanyasu (katikati) akiwa amekaa na wananchi wa kata ya Ihanamiro huku
akiwa akiwa anazungumza nao kabla ya kikao cha ndani kuanza.
……………………….
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema
Halmashauri ya mji wa Geita hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu tayari
imeshatoa mkopo wa Shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya wakinamama, vijana
na walemavu kwa lengo la kutimiza adhima ya Serikali ya awamu ya tano
chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli.
Amesema lengo la kutoa mkopo huo ni
kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira na kuweza kuinua kipato cha
wananchi kwa kunufaika na miradi mbalimbali na hatimae kuweza kujikwamua
kiuchumi.
Hayo ameyasema kwenye mkutano wakati
akizungumza na wananchi wake kuhusu ahadi mbalimbali alizozitekeleza
ikiwemo ya kutoa mkopo wa shilingi bilioni 1.6 kwa vikundi mbalimbali
kwa lengo la kupunguza umasikini katika jamii katika mkutano huo
uliofanyika katika kata ya Ihanamiro wilaya ya Geita mkoani Geita.
Mhe.Kanyasu amewaeleza wananchi hao kuwa
kutokana na uhusiano mzuri uliopo miongoni mwa madiwani katika
Halmashauri hiyo wameweza kutoa mkopo huo. Hata hivyo amesema kuwa
mikopo hiyo itasaidia katika uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo
ambavyo vitasaidia kutengeneza ajira na kukuza uchumi
Akizungumza katika mkutano
huo,Mhe.Kanyasu amesema anajisika fahali ya kutoa mikopo hiyo kwa
vikundi ikiwa ni moja ahadi alizozitimiza za kuhakikisha mwananchi wake
wanajihusisha kwenye shughuli za kiuchumi ili kupunguza umasikini
kuanzia ngazi ya familia hadi taifa
Amesema kuwa kutokana na changamoto
zilizoko katika taasisi za fedha, ambazo hutoa mikopo kwa riba kubwa na
kuhitaji dhamana ya nyumba na ardhi jambo ambalo linawakwamisha
wakopaji hivyo serikali imeamua kutoa mikopo ya masharti nafuu.
Aidha amesema mikopo hiyo itawasaidia makundi hayo kuweza kuongeza mitaji na kutoa ajira ndani ya jamii.
Aidha, Mhe, Kanyasu amesema katika awamu
ya pili ya utoaji mkopo wataongeza viwango vya mikopo kwenye vikundi
ambapo kila kikundi kitakuwa na uwezo wa kukopeshwa hadi kufikia
shilingi milioni 20 tofauti na ilivyokuwa awali
Kwa upande wake, Diwani wa kata ya
Ihanamiro, Mhe. Joseph Lugaira amemueleza Mbunge huyo kuwa katika kata
hiyo jumla ya vikundi 19 vimenufaika na mkopo huo kwa kuanzisha shughuli
za kiuchumi.
Amesema vikundi hivyo vimekuwa vikifanya
shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo biashara pamoja na kilimo ambapo
anaamini wataweza kupata faida pamoja na kurejesha mkopo huo na kukopa
tena.
Naye Diwani wa viti maalum, Mhe. Suzana
Mashala amewahimiza wanawake wasiogope kukopa kwani hawawezi
kujiendeleza kiuchumi pasipo kukopa.
Vile vile, Diwani huyo alitumia fursa
hiyo kuwahimiza wanawake waliokopa wajitahidi kurejesha mikopo hiyo
mapema ili mikopo hiyo iweze kuwasaidia watu wengine lengo likiwa ni
kuondokana na umasikini.
Kwa upande wake, Emalio Nyangabo ambaye
ni kiongozi wa Kikundi cha Tuinuane, amesema walipokea mkopo ambao
umewasaidia kuinuka kiuchumi, na kuwawezesha kufanya shughuli za
uzalishaji mali na kuachana na kujihususha na vitendo visivyofaa katika
jamii
Naye, Godson Maduka ambaye ni miongoni
mwa vijana walionufaika wa mkopo huo amesema mkopo huo umewasaidia
vijana wengi kujiepusha kujiingiza kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya
na unywaji wa pombe kupita kiasi.
0 comments:
Post a Comment