Naibu
Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile akipimwa joto la mwili na
mhudumu wa uwanja wa ndege mara baada ya kufika katika mkoa wa Kigoma
ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.Naibu
Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile akimpima joto la mwili mkuu wa
Wilaya ya Kigoma Bw. Samson Anga wakati alipotembelea bandari ya Kigoma
kuona hali ya utayari wa mkoa huo katika kukabiliana na ugonjwa wa
Ebola.Naibu
Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile akioneshwa vifaa vya kujikinga
na Ebola kutoka kwa mhudumu wa afya wa bandari ndogo ya Kibirizi Mkoani
Kigoma wakati wa ziara yake mkoani humo kuangalia utayari wa mkoa katika
kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.Naibu
Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile (Kulia) akitoa maelekezo kwa
Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Paul Chaote jinsi ya kuweka vifaa na
kupangiliana hema (Isolation centre) kwa ajili ya wagonjwa wa Ebola.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga.Naibu
Waziri Dkt. Faustine Ndugulile akikagua dawa na vifaa vinavyotumika
katika kutibu mgonjwa wa Ebola, kulia ni Dkt. Praygod Swai wa Zahanati
ya Bangwe iliyotengwa maalum kwa ajili ya kutibu wagonjwa wa Ebola
akimuonesha vifaa hivyo.Hema lilotengwa kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa Ebola katika bandari ndogo ya Kibirizi ikiyoko mkoani Kigoma.
……………………..
Na WAJMW-Kigoma
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo ametembelea baadhi
ya maeneo ya Mkoa wa Kigoma kuona utayari wa mkoa huo katika kukabiliana
na ugonjwa wa Ebola.
Dkt. Ndugulile ametembelea maeneo ya
Bandari kuu ya Mkoa, Uwanja wa ndege, bandari ndogo ya Kibirizi na
Zahanati ya Bangwe ambayo imetengwa maalumu kwa ajili ya kutoa matibabu
kwa mtu atakayebainika kuwa na virusi vya Ebola.
Naibu Waziri ameonekana kutoridhishwa na
utayari wa Mkoa katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini huku
akiitaka timu iliyoandaliwa chini ya Mkuu wa Wilaya Samson Anga na
Mganga Mkuu wa Mkoa Paul Chaote kuendelea kutoa mafunzo kwa timu
iliyoandaliwa jinsi ya kujikinga na kutoa huduma kwa mgonjwa
atakayebainika.
“Hatuna mgonjwa wa Ebola ndani ya nchi,
lakini kutokana na hali ya ugonjwa huu katika nchi jirani kuna umuhimu
wa sisi kama nchi kuendelea kujipanga na kuhakikisha kwamba mifumo yetu
yote imekaa vizuri kipindi mgonjwa atakapojitokeza, hivyo nakuomba Mkuu
wa Wilaya na Mganga Mkuu wa mkoa kuendelea kusimamia hili”. Amesema Dkt.
Ndugulile.
Mapungufu aliyobaini Dkt. Ndugulile ni
pamoja na wahudumu kutozingatia kanuni walizofunzwa juu ya kujikinga na
maambukizi pindi watakapokua wakihudumia mgonjwa, kutokua na vifaa vya
kutosha kwa ajili ya wagonjwa wa Ebola kama vitanda kwenye vituo vya
Isolation na watumishi kutokua na uelewa na utayari wa kutosha kwa ajili
ya kukabiliana na ugonjwa huu.
Dkt. Ndugulile yupo Mkoani Kigoma kwa
ziara ya siku tatu ambapo pamoja na maeneo mengine atatembelea mpaka wa
Manyovu ili kuona hali ya utayari ya mpaka huo kwa ajili ya kukabiliana
na ugonjwa wa Ebola na kisha atatembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Kigoma.
0 comments:
Post a Comment