Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent
Bashungwa akizungumza wakati wa hafla ya kufunga Manoesho ya 43 ya
Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika
Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere leo Alhamisi (Julai 11, 2019).
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akimkabidhi cheti cha ushindi
mmoja wa washiriki wa makampuni kutoka nchini Rwanda, wakati wa hafla
kufunga Manoesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF)
leo Alhamisi (Julai 11, 2019)yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu
Julius Nyerere.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi, Balozi Seif Alli Idd akimkabidhi cheti cha ushindi mmoja wa
washiriki wa makampuni yaliyoshiriki katika Maonesho ya 43 ya Biashara
ya Kimataifa Dar es Salaam wakati hafla kufunga maonesho hay oleo
Alhamisi (Julai 11, 2019) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu
Julius Nyerere.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Alli Idd akimkabidhi cheti cha ushindi
Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi Dorina
Kaaya wakati wakati wa hafla kufunga Manoesho ya 43 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) leo Alhamisi (Julai 11,
2019)yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Alli Idd akimkabidhi cheti cha ushindi
mmoja wa washiriki kutoka Kampuni ya uzalishaji maziwa ya Asasi Diaries
wakati wakati wa hafla kufunga Manoesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa
ya Dar es Salaam (DITF) leo Alhamisi (Julai 11, 2019)yanayoendelea
katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
(PICHA NA PASCHAL DOTTO-MAELEZO)
…………………………
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
DAR ES SALAAM
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi ameitaka Mamlaka ya Maendeleo ya
Biashara Tanzania (TANTRADE) kuendelea kuimaisha mitandao na mifumo ya
biashara nchini ili kuwawezesha wafanyabiashara wa Tanzania kuweza kuwa
na uhakika wa masoko bora ya bidhaa za ndani na nje ya nchi.
Akifunga Maonesho ya 43 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) leo Alhamisi (Julai 11, 2019) Balozi
Idd alisema Maonesho hayo ya mwaka huu yameonesha dhamira na mwelekeo wa
Serikali katika kutumia fursa biashara na viwanda katika kujenga uchumi
imara pamoja na kutengeneza ajira kwa wananchi.
Balozi Idd alisema ni wajibu wa TANTRADE
kutumia fursa za uwepo wa makampuni ya wazalishaji, wauzaji na
wafanyabiashara kutoka nje wanaoshiriki katika maonesho hayo kuweza
kujenga mitandao imara ya mahusiano na ushirikiano kwa wafanyabiashara
wa ndani ili kuweza kuwatafutia masoko ya bidhaa zao ambazo kwa sasa
zimeanza kuzalishwa katika viwango bora nchini.
“Nawapongeza TANTRADE kwa juhudi zenu za
kuanzia klinilki za biashara, na hili limewezesha wafanyabiashara wetu
kuweza kukutana na wanunuzi mbalimbali ambao huweza kuwapa uzoefu wa
namna bora zaidi ya kuzalisha bidhaa zenye kukithi viwango na ubora
unaotakiwa” alisema Balozi Idd.
Aidha Balozi Idd alisema Serikali kwa
sasa inatekeleza Mpango Kazi wa Kuboresha Mfumo Udhibiti wa Biashara
Nchini (Blue Print), ambao umekusudia kuondoa changamoto mbalimbali za
wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, hivyo aliitaka TANTRADE
kushirikiana na wadau na wazalishaji wa sekta binafsi ili kuiwezesha
sekta ya biashara kuvutia wawekezaji wengi zaidi.
Kwa mujibu wa Balozi Iddi pia aliitaka
TANTRADE kuweka utaratibu wa kufuatilia oda za maombi mbalimbali
zinazotolewa na wafanyabiashara kutoka nje ya nchi ili kuendelea kupanua
wigo wa soko la bidhaa za Tanzania nje ya nchi ambalo kwa sasa
limeendelea kupanuka kutokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na
Serikali.
Balozi alisema ni wajibu wa Watanzania
kujenga utamaduni wa kuthamini bidhaa za ndani ili kuziwesha kupata
masoko ya uhakika kwa kuwa kwa kufanya hivyo kutatoa fursa ya kuweza
kutambulika kwa haraka pamoja na kumudu changamoto ya ushindani wa
masoko ya bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi.
Alisema kuwa maonesho hayo ya 43
yamethibitisha uwezo wa wafanyabiashara wa Tanzania katika kutengeneza
na kuzalisha bidhaa mbalimbali kwani idadi ya washirki wa maonesho
kutoka nje ya nchi imeweza kuongezeka kutoka makampuni kutoka nje 2956
mwaka 2018 hadi kufikia 3250 mwaka 2019, hivyo kudhibitisha uwezo wa
serikali katika kusimamia sekta ya biashara nchini.
Balozi Idd anasema kuwa Makampuni ya
wafanyabiashara ya Tanzania yaliyoshiriki maonesho hayo yanapaswa kupata
uzoefu na uelewa mkubwa katika namna bora zaidi ya kusimamia na
kuratibu sekta ya biashara nchini katika viwango bora ili kuweza
kutengeneza masoko ya uhakika katika nchi za nje.
Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na
Biashara, Innocent Bashungwa alisema Serikali imeendelea kuboresha
mazingira ya biashara nchini ikiwemo kuanza kufanya mapitio ya sera na
sheria mbalimbali ambazo awali zilikuwa zikileta changamoto mbalimbali
kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa katika kuhakikisha kuwa
sekta ya viwanda na biashara inaleta tija katika ukuaji uchumi nchini,
Serikali imekusudia kuweka msisitizo katika kujenga uchumi jumuishi kwa
kuziweka sekta ya uvuvi, kilimo na mifugo kuwa kipaumbele muhimu katika
kuzitumia rasilimali mbalimbali zilizopo katika sekta hizo katika
kutengeneza ajira kwa wananchi walio wengi.
0 comments:
Post a Comment