METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, January 11, 2021

BODABODA BUKOBA WAIANGUKIA SERIKALI MIKATABA UMIZA,RC ATOA SIKU 7 KUSHUGHULIKIA SUALAHILO

Mkuu  wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali  Marco Gaguti akiwahutubia madereva bodabodaManispaa ya Bukoba wakati alipofika maeneo ya ofisi za ushirika wa bodaboda kwa lengo la kuwasalimia.

Madereva bodaboda manispaa ya Bukoba ambao  ni wanachama wa ushirika huo   wakimsikiliza mkuu  wa koa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti wakati  alipokuwa akiwahutubia.

Waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda manispaa ya Bukoba kupitia ushirika wao, wameiomba serikali kuingilia kati suala  la mikataba umiza ambayo hailengi kuwanufaisha madereva hao na badala yake huwarudisha nyuma na kujikuta wanaendelea na maisha ya utegemezi.

Ombi hilo limetolewa na mwenyekiti wa madereva bodaboda Manispaa ya Bukoba Abdul Salumu Mashankala kwa mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti ambaye pia ni mlezi wa ushirika huo alipofanya ziara ya kuwatembelea na kutaka kujua maendeleo yao leo januari 11,2021, ambapo amesema kuwa pamoja na vijana wengi wanaojishughulisha na kazi hiyo wanakumbana na changamoto ya mikataba ambayo inamunufaisha zaidi mmiliki wa chombo.

Mashankala ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa ushirika huo ulianzishwa mwezi novemba mwaka jana ukiwa na wananchama waanzzilishi 130 umefanikiwa kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 3 ikiwa na ada ya kila mwananchama ya kila siku ambapo kila mwanachama hutoa shilingi 500.

Aidha amemshukuru naibu waziri  wa nishati  na mbunge wa jimbo la  Bukoba mjini Mhe. Stiphen  Byabato ambaye ameonekana kuwaunga mkono licha ya yeye kuwa mwananchama lakini amesema kuwa aliwapati computer set pamoja na kuahidi  kumlipa muhudumu wa ofisi yao kwa mwaka mzima.

Ameongeza kuwa vijana wengi wa bodaboda wamekuwa wakishindwa kumaliza mikataba yao  kutokana na  mikataba hiyo kuonyesha kuwanufaisha wamiliki wa vyombo hivyo nap engine kupelekea kunyang’anywa pikipiki kwa kushindwa kumalizia marejesho. 

Kutokana na ombi la bodaboda hoa, mkuu wa mkoa Kagera ametoa muda wa wiki moja kwa mwenyekiti  huyo  kumpelekea orodha ya majina ya bodaboda ambao wako kwenye mikataba ili kuweza kuipitia pamoja na wamiliki wa vyombo hivyo ili kuweza kufikia muafaka wa namna gan mikataba hiy inawanufaisha watu wote wawili.

Hata hivyo amewataka bodaboda hao kuongeza kiasi cha ada kutoka shilingi 500 hadi shilingi 1000 kwa siku ili kuweza kutunisha mfuko wao na kuweza kuleta maana halisi  ya ushirika.

Gaguti ameongeza kuwa lengo kuu  la kuanzishwa kwa ushirika huo ni kutaka kuwaunganisha poamoja vijana hao na kuweza kuwainua kiuchumi kutoka kuendelea kutegemea kuendesha pikipiki za watu na badala yake kila mmmoja awe na pikipiki yake.

Kwaupande wake mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Kagera RTO Denis Kunyanja amesema kuwa muunganiko wa vijana hao wa bodaboda unwapa ulahisi wa kuweza kupewa elimu ya usalama barabarani na kuweza kupunguza ajali za barabarani.

Kunyanja ameongeza kuwa kujiunga kwa vijana hao kunatoa mwanya kwa utii wa sheria bila shuruti ambapo amewataka vijana wengine kujiunga ili kuweza kutii sheria bila shuruti.

Kwaupande wao baadhi ya bodaboda wamesema kuwa ushirika huo unawanufaisha kwa kuwezza kujulikana na kumaliza matatzo mbalimbali yanayowakabili.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com