Waziri wa Fedha na Mipango,Dk. Philip
Mpango, akipokea gawio la shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali, ikiwa ni
sehemu ya faida ya benki ya TPB kwa mwaka 2017/2018 kutoka kwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Dkt.Edmund Mndolwa.
Waziri wa Fedha na Mipango,Dk.Philip
Mpango,akizungumza na wafanyakazi na wanahisa wakati wa kupokea gawio
la shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida ya benki
ya TPB kwa mwaka 2017/2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa
Benki ya TPB Dkt.Edmund Mndolwa,akizungumza mara baada ya kukabidhi
gawio la shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida ya
benki ya TPB kwa mwaka 2017/2018
Mtendaji Mkuu wa Benki ya TBP,Sabasaba Moshing,akiongea na wafanyakazi na wanahisa wakati wa kutoa gawio la shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida ya benki ya TPB kwa mwaka 2017/2018 .
Waziri wa Fedha na Mipango,Dk. Philip
Mpango, akiteta jambo na Mtendaji Mkuu wa Benki ya TBP,Sabasaba Moshing
wa kwanza kulia na wa (katikati) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
wa Benki ya TPB Dkt.Edmund Mndolwa mara baada ya kupokea gawio la shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida ya benki ya TPB kwa mwaka 2017/2018 .
Waziri wa Fedha na Mipango,Dk. Philip Mpango, akiwa katika picha ya pamoja na wanahisa mara baada ya kupokea gawio la shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida ya benki ya TPB kwa mwaka 2017/2018 .
Waziri wa Fedha na Mipango,Dk. Philip
Mpango, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya TPB
mara baada ya kupokea gawio la shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida ya benki ya TPB kwa mwaka 2017/2018 .
………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
BENKI ya Posta Nchini TPB leo imekabidhi
gawio la Shilingi bilioni 1.2 kwa Serikali ya Tanzania pamoja na
Wanahisa wengine wa benki hiyo.
Gawio hilo limetokana na faida ambayo benki hiyo imeipata kutokana na shughuli zake katika kipindi cha mwaka 2017/2018.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya
kukabidhi gawio hilo iliyofanyika kwenye ofisi za Wizara ya Fedha na
Mipango mjini Dodoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB
Dkt. Edmund Mndolwa alisema benki ya TPB imefanya vizuri mwaka jana kwa
kupata faida ya Shilingi bilioni 17, na hivyo kuweza kutoa gawio la
shilingi Bilioni moja na Milioni Mia Mbili (1.2 bilioni) kwa Serikali
pamoja na Wanahisa wake.
“Mimi kama Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya
TPB najisikia faraja kusimamia benki inayoendelea kufanya vizuri
miongoni mwa mabenki takriban 54 yaliyopo sokoni hivi sasa.
Dkt.Mndolwa amesema kuwa Wanahisa
wanaridhishwa na utendaji wa benki kwa kipindi hicho kwani benki
ilifanikiwa kupata faida ya kiasi cha shilingi bilioni 17.2 kabla ya
kodi.
”Nichukue fursa hii kuwashukuru sana wateja wetu ambao wameendelea kutuamini kwa kutumia huduma zetu kwa wingi.
”Ahadi yetu kwao ni kwamba tutaendelea kutoa huduma bora na zenye kukidhi mahitaji yao”, alisema Dkt. Mndolwa
Akipokea gawio hilo, Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango aliipongeza benki ya TPB kwa kuendelea
kufanya vizuri miongoni mwa mabenki takriban 50 yaliyopo nchini.
“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati
kwa uongozi wa Benki ya TPB kwa gawio hili la shilingi bilioni Moja
mlilolitoa kwa Serikali.
”Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Benki
hii kufanya hivyo, na kwasababu hiyo basi, nitoe pongezi kubwa na za
dhati kwa uongozi wa TPB kwa gawio hili. Kutoa kwenu gawio kwa wanahisa
wenu kunaashiria kwamba Benki ya TPB imeendelea kufanya vizuri
kiutendaji, na hii inatia moyo na kutoa hamasa kwa wanahisa tunaomiliki
hisa kwenya benki yenu.
Hii ni ishara pia kuwa taasisi
zinazomilikiwa na Serikali zinaweza kujiendesha kwa ufanisi na kwa
faida, kiasi cha kuweza kutoa ushindani kwa taasisi nyingine za
binafsi”, amesema Waziri Mpango
Waziri Mpango pia alitumia fursa hiyo
kutoa wito kwa taasisi za Serikali kutumia huduma za kibenki kutoka
benki hiyo kupitia matawi yake yaliyoenea nchi nzima ili kuiunga mkono.
“Napenda kutoa wito kwa taasisi zingine
za umma zinazotaka huduma za Kibenki kote nchini Tanzania na Watanzania
wote kwa ujumla kutumia huduma za Benki ya TPB zilizoko mikoa yote
nchini Tanzania.
Benki ya TPB yenye matawi 75 nchi nzima
inao wanahisa sita ambao ni Serikari ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shirika la Posta, Saccos ya
Posta na Simu, Workers Compensation Fund pamoja na PSSSF.
0 comments:
Post a Comment