Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limethibitisha Tanzania kuingiza na timu
nne katika mashindano ya klabu barani kwa msimu wa 2019/2020.
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo imesema kwamba timu
mbili zitashiriki katika Ligi ya Mabingwa na nyingine mbili zitashiriki
Kombe la Shirikisho.
Nafasi hiyo kwa Tanzania imekuja baada ya kuwa katika nafasi 12 bora kwenye viwango vya ubora vya CAF.
Kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu zilizofanyiwa marekebisho na Kamati ya
Utendaji baada ya kupatikana nafasi nne (4) timu za Tanzania
zitakazowakilisha kwenye mashindano hayo ni Simba na Young Africans,
maarufu Yanga Ligi ya Mabingwa (CAF CL),Azam FC na KMC Kombe la
Shirikisho (CAF CC).
KMC atawakilisha Kombe la Shirikisho kwa
mujibu wa Kanuni hiyo ambayo inatamka kama timu iliyomaliza nafasi ya 3
itakua ndio bingwa wa Kombe la FA basi mshindi wa 4 anapata nafasi ya
kucheza Kombe la Shirikisho kwasababu bingwa wa FA anaiwakilisha nchi
kwenye mashindano hayo.
Tayari CAF imefungua dirisha kwa Mashirikisho kusajili timu kupitia mtandao wa CMS.
Mwisho wa usajili ni Juni 30,2019 ambapo TFF inatakiwa iwe imesajili
timu zitakazoshiriki kwenye mashindano ya Kimataifa msimu wa 2019/2020.
Rais wa TFF Wallace Karia amezitaka klabu zilizopat nafasi kusajili kwa
umakini na kujiandaa kwa Mashindano ya CAF ili kutopoteza nafasi ya
kuingiza timu nne katika mashindano ya CAF
0 comments:
Post a Comment