Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisisitiza jambo wakati akifungua kikao kazi cha wadau kuhusu marekebisho ya sera ya Kilimo kinachofanyika Jijini Dodoma katika ukumbi wa Morena tarehe 13 Juni 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha wadau kuhusu marekebisho ya sera ya Kilimo kinachofanyika Jijini Dodoma katika ukumbi wa Morena tarehe 13 Juni 2019.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisisitiza jambo wakati akifungua kikao kazi cha wadau kuhusu marekebisho ya sera ya Kilimo kinachofanyika Jijini Dodoma katika ukumbi wa Morena tarehe 13 Juni 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Wizara
mbalimbali zimeanza ushirikishwaji wa kujadiliana kuhusu utekelezaji wa Sera ya
Kilimo ya Taifa ya Mwaka 2013 na kutoa maoni yao kuhusu mapendekezo ya
kurekebisha Sera hiyo.
Katibu Mkuu Wizara
ya Kilimo, Mhandisi Mathew John Mtigumwe ameyasema hayo wakati
akifungua kikao kazi cha wadau kuhusu marekebisho ya sera ya Kilimo
kinachofanyika Jijini Dodoma katika ukumbi wa Morena tarehe 13 Juni 2019.
Mhandisi Mtigumwe amesema kuwa Maboresho hayo yanalenga kuhuisha
shughuli za kilimo ili ziendane na mahitaji halisi ya nchi ikiwa ni pamoja
maendeleo ya viwanda.
Alisema, timu ya Wataalamu ya Wizara ya Kilimo inaendelea na ukusanyaji
wa maoni kutoka kwa Wadau maeneo mbalimbali ya nchi ikizingatia pia ushiriki wa
makundi mbalimbali ya Kijamii.
Katika
kikao kazi hicho Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa fursa hiyo ya kushirikishwa
katika mchakato wa mapitio ya marekebisho ya Sera ya Kilimo, ni heshima kubwa kwa
wadau hao. “Hivyo, nawasihi wadau wote mshiriki kikamilifu kutoa maoni yenu kwa
uwazi na uhuru ili kuakisi uaminifu mliopewa na Wizara ya Kilimo. Aidha, maoni
yenu ni muhimu katika maboresho ya Sera ya Kilimo yatakayochochea ukuaji wa
sekta ya kilimo ambayo hutegemeana na sekta nyingine katika ukuaji wa uchumi
kwa lengo la kufikia uchumi wa kati” Alikaririwa Mhandisi Mtigumwe
Kadhalika
alisema pamoja na mambo mengine lakini wadau watapata fursa ya kutambua
jitihada za Serikali zinazoendelea katika kurekebisha Sera ya Kilimo ya Mwaka
2013 na kutoa maoni yao kwa uwazi na uhuru katika marekebisho ya Sera yanayopendekezwa.
Aidha,
Mhandisi Mtigumwe amesema kuwa pamoja na ukweli kwamba, Wizara imeandaa Rasimu
ya Taarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Kilimo ya Taifa ya Mwaka, 2013 pamoja na uchambuzi
unaoainisha mapungufu ya awali (gap
analysis). Hata hivyo, kikao hicho kitatoa mwanga zaidi wa mapungufu
yaliyopo na kuyaainisha kabla ya kuendelea katika hatua zinazofuata.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment