Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo, Felix Tshisekedi kesho Juni 13 anatarajia kufanya ziara ya
kikazi kwa siku mbili nchini Tanzania na kupokelewa na mwenyeji wake
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli.
Akitoa taarifa ya ugeni huo, Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema Rais Felix
Tshisekedi atawasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere
Majira ya Mchana na baada ya kuwasili ataelekea Ikuku Dar es salaam
ambapo atafanya mazungumzo na Rais Dkt. John Magufuli kuhusu mambo
mbalimbali ikiwemo jinsi ya kuimarisha uchumi na maendeleo.
RC Makonda amesema ugeni wa
viongozi mbalimbali nchini ni matokeo ya uongozi imara na thabiti wa
Rais Dkt. John Magufuli katika usimamizi wa Amani, usalama, maendeleo na
uwepo wa diplomasia imara
0 comments:
Post a Comment