Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya
Vifaa saidizi kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu na Cherehani kwa ajili ya
wakina Mama zilizotolewa na Balozi wa China Nchini Bi. Wang Ke wakati wa
hafla hiyo iliyofanyika leo tarehe 26 Juni, 2019 katika Ofisi ndogo za
Ubalozi huo zilizopo Jijini Dodoma.
Balozi wa China Nchini Tanzania Bi. Wang
Ke akielezea namna Serikali ya China imekuwa ikisaidia masuala
mbalimbali nchini wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Vifaa saidizi
kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu na Cherehani kwa ajili ya wakina Mama
iliyofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama akiteta jambo na Balozi wa China Nchini Tanzania Bi.
Wang Ke wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Vifaa saidizi kwa ajili
ya Watu wenye Ulemavu na Cherehani kwa ajili ya wakina Mama iliyofanyika
Jijini Dodoma katika Ofisi ndogo za Ubalozi huo Juni 26, 2019.
Baadhi ya Viongozi wakimsikiliza Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama. Kushoto ni Balozi
wa China Nchini Tanzania Bi. Wang Ke, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki, Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Mhe.
Stella Ikupa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mhe. Fatma
Toufiq(kulia).
Baadhi ya Wadau walioshiriki kwenye hafla
hiyo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
(hayupo pichani).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama (kushoto) pamoja na Balozi wa China Nchini Tanzania Bi.
Wang Ke (katikati) wakimkabidhi Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (kulia) Kiti
Mwendo “Wheelchair” ikiwa ni sehemu ya maabidhiano wakati wa hafla hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama (wa pili kutoka kulia) akimkabidhi Fimbo Nyeupe “White
Cane” mmoja wa wanafunzi wasioona kutoka Shule ya Msingi ya Buigiri. Wa
tano kutoka kulia ni Balozi wa China Nchini Tanzania Bi. Wang Ke. Kulia
ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye
Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa.
Balozi wa China
Nchini Tanzania Bi. Wang Ke akimkabidhi cherehani kwa Mbunge wa Viti
Maalum Mkoa wa Dodoma, Mhe. Fatma Toufiq wakati wa hafla hiyo
iliyofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki (wa tatu
kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa China Nchini
Tanzania Bi. Wang Ke (katikati). Wa tatu kutoka kushoto ni Naibu Waziri,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella
Ikupa. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza Mhe. Kemilembe
Lwota na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mhe. Fatma Toufiq.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
……………………
NA; Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama amepokea cherehani na vifaa siadizi kwa ajili ya Watu
wenye Ulemavu vilivyotolewa na Ubalozi wa China nchini.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi ya
makabidhiano iliyofanyika katika ofisi ndogo za ubalozi huo zilizopo
Jijini Dodoma, Waziri Mhagama alieleza kuwa Serikali inatambua haki za
Watu wenye Ulemavu nchini hivyo imekuwa ikishirikiana na wadau
mbalimbali wa maendeleo ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki
zao stahiki ikiwemo kuwapatia vifaa saidizi.
“Vifaa saidizi ni muhimu kwa kundi hilo
maalumu kwa kuwa vinawawezesha kumudu mazingira yanayowazunguka na
kuwasaidia kufanya shughuli zao za kila siku bila kukabiliana na
changamoto,” alisema Mhe. Mhagama
Alieleza kuwa kutokana na vifaa hivyo
kuwa ni ghali na upatikanaji wake umekuwa mgumu na kupelekea watu wenye
ulemavu kushindwa kuvinunua, Serikali imeendelea kutenga bajeti kwa
ajili ya kununua vifaa hivyo.
Aliongeza kuwa, katika ujenzi wa uchumi
wa viwanda Serikali kupitia Shirika la kuhudumia viwanda Vidogovidogo
(SIDO) kushirikiana na wadau imejipanga kuimarisha utengeneza wa baadhi
ya vifaa hivyo, vitakavyokuwa vinapatikana hapa nchini.
Aidha alitoa wito kwa jamii kubadili
mtazamo na fikra potofu juu ya watu wenye ulemavu, bali watambue kundi
hilo linaweza na linamchango mkubwa katika jamii na nchi kwa ujumla.
Kwa upande wake, Balozi wa China nchini
Tanzania, Bi. Wang Ke alisema kuwa Serikali ya China itaendelea
kuimarisha ushirikiano wake na Serikali ya Tanzania katika nyanja
mbalimbali pamoja na kuendelea kutoa misaada kwa ajili ya wenye uhitaji.
Naye Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa aliwataka wadau
ndani na nje ya nchi kuendelea kujitokeza na kusaidia makundi yenye
uhitaji maalumu, kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusaidia
masuala ya Watu wenye Ulemavu.
Katika hafla hiyo pia aliudhuria Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.
Angellah Kairuki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mhe. Fatma
Toufiq na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza Mhe. Kemilembe Lwota.
0 comments:
Post a Comment