METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, June 10, 2019

ULEGA AFUNGUA SOKO LA SAMAKI LA NYAKALIRO LILILOPO BUCHOSA MKOANI MWANZA

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ,akizungumza wakati wa kufungua  soko la samaki  la Nyakaliro lililopo Halmashauri ya Buchosa Mkoani Mwanza.

Hili ndiyo jengo la soko la Nyakalilo lililofunguliwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega

………………….

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega  amefungua soko la samaki  la Nyakaliro lililopo Halmashauri ya Buchosa Mkoani Mwanza.

Soko hilo  lililokuwa limefungwa miaka mitatu iliyopita kutokana na kutokuwa na usimamizi mzuri ikiwemo uzalishaji mdogo wa samaki na dagaa pamoja na mianya ya utoroshaji wa mazao ya uvuvi.

Ulega alisema, Rais amewatengenezea miundombinu ya soko kwa maslahi mapana ya taifa kwa kutaka wananchi wafanye kazi.

“Sasa tumeisha weka mfumo mzuri wa usimamizi ndio maana leo tumefungua soko hili, ili mapato ya Serikali yaweze kukusanywa kwa haki na wananchi wa maeneo haya waweze kufanya shughuli za kujiingizia kipato,” alisema Ulega.

Hivyo alimuagiza,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa Crispin Luanda, kufanyia maboresho haraka soko hilo hili wananchi waanze kufanyabiashara huku  akisisitiza kuwa mfanyabiashara akiwa amekata vibali kutoka eneo moja anaruhusiwa kufanya biashara sehemu yoyote bila kubuguziwa na jambo hilo atalisimamia.

Pia aliutaka uongozi wa uvuvi Kanda ya Ziwa leo( jumatatu) kumpeleka ofisa ambaye atakuwa anasimamia ukaguzi na kutoa vibali katika soko hilo,pamoja na DED Buchosa kutafuta mawakala wa huduma za kifedha sokoni hapo ili kuwapa urahisi wafanyabiashara.

Aidha alitumia fursa hiyo kwa kusema, ataka na wataalamu wa uvuvi ili kupitia na kuangalia sheria inayokataza samaki ambaye ajachakatwa kuuzwa nje ya nchi kwa maslahi mapana ya taifa.

Ili waweze kuruhusu ata wale ambao hawawezi kuuza viwandani kufanyabiashara, hivyo  kwa kufanya utafiti na kuona kama samaki akiuzwa nje bila kuchakatwa mvuvi atapata mapato na taifa pia.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Buchosa Shija Lyella alisema,wananchi wanashukuru kwa kufunguliwa soko hill  la Nyakaliro  ambalo ni chanzo muhimu cha mapato ya halmashauri hiyo na kichocheo cha uchumi kwa wadau wa sekta ya uvuvi ndani na nje.

“Lengo ni kutoa huduma ya soko kwa wadau Wa uvuvi wa dagaa na samaki wakavu,kuiwezesha halmashauri kukusanya mapato yatokanayo na ushuru wa mazao ya uvuvi,kuchochea Biashara ndogo ndogo pamoja na kutoa ajira kwa wananchi Wa maeneo husika.Kijiografia soko hili lina nafasi kubwa zaidi ya kuwa la kimataifa kwa sababu za uzalishaji wa mazao ya uvuvi unaokadiriwa kuwa tani 4000 za dagaa na 2600 za samaki kwa mwaka,”alisema Lyella.

Naye Mbunge wa Jimbo la Buchosa Dkt.Charles Tizeba alimuomba, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega aiagize Halmashauri ya Chato kuacha kuwasumbua wafanyabiashara wanaonunua samaki kutoka katika soko la Nyakaliro pamoja na kuruhusu uuzwaji wa samaki nje ambao hawajachakatwa.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com