Mkuu
wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiangalia ramani ya upanuzi wa Kituo cha
Afya Bwisya kilichopo katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu
wa Mkoa Mwanza, John Mongella leo Ijumaa Juni 07, 2019 amekagua
maendeleo ya upanuzi na ujenzi wa Kituo cha Afya Bwisya kilichopo
wilayani Ukerewe na kulidhishwa na ujenzi wake ambao umefikia asilimia
95 kwa mujibu wa mkandarasi.
Upanuzi
wa Kituo hicho kwa hadhi ya Hospitali ni sehemu ya agizo la Rais Dkt.
John Pombe Magufuli alilolitoa baada ya ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere
iliyotokea Septemba 20, 2018 ambapo alielekeza sehemu ya fedha za
rambirambi ya ajali hiyo (Milioni 800) zitumike kufanya shughuli hiyo.
Mongella
amesema ukarabati huo ulipaswa kukamilika mwezi Machi mwaka huu lakini
umechelewa kutokana na changamoto ya miundombinu ya usafiri kwani baadhi
ya vifaa ujenzi vinatoka jijini Mwanza na kusafirisha kwa njia ya maji
hivyo matarajioni ni mkandarasi kampuni ya Suma JKT kukamilisha kazi
hiyo mwishoni mwa mwezi huu.
Pia
amekagua maendeleo ya Shule ya Sekondari Nyamanga iliyopo kisiwani
Ukara aliyoiwekea jiwe la msingi la ujenzi Mei 02, 2019 na kuelekeza
maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vyumba vya madarasa kukamilika kwa
wakati ili kutoa fursa kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza walioanza
masomo shuleni hapo kuelendelea vyema na masomo yao.
Aidha
Mongella amekagua matayarisho ya ujenzi wa uzio, mnara na makaburi ya
baadhi ya abiria wa Kivuko cha MV. Nyerere waliozikwa katika malalo ya
pamoja eneo la Bwisya kisiwani Ukara na kuelekeza Suma JKT kukamilisha
pia shughuli hiyo kwa wakati.
Itakumbukwa
kwamba Novemba 17, 2018 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo alizindua rasmi ujenzi wa
miundombinu katika Kituo hicho unaofanywa na kampuni ya SUMA JKT chini
ya usimamizi wa Kamati Maalum iliyoundwa na Mongella.
Kukamilika
kwa upanuzi wa Kituo cha Afya Bwisya, kutaondoa adha kwa wananchi zaidi
ya elfu thelathini waliokuwa wakivuka maji kwenda Mjini Ukerewe ama
Jijini Mwanza kufuata huduma za afya.
Sehemu ya majengo yaliyojengwa kwenye Kituo cha Afya Bwisya wilayani Ukara.
Tenki la kuhifadhia maji katika Kituio cha Afya Bwisya.
Majengo yaliyojengwa kwenye
Kituo cha Afya Bwisya ni pamoja na nyumba ya mtumishi, maabara, wodi ya
wazazi, jengo la upasuaji na jengo la kuhifahia maiti.
Upanuzi
wa Kituo cha Afya Bwisya umefikia asilimia 95 ambapo asilimia tano
zilizosalia zinatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 17, 2019.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akikagua maendeleo ya upanuzi wa Kituo cha Afya Bwisya kilichopo Ukara wilayani Ukerewe.
Mkuu
wa Mkoa Mwanza, John Mongella aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule
hii Mei 02, 2019 na kufufua ujenzi wake ambao ulikuwa unasua sua tangu
mwaka 2014.
Mkuu
wa Mkoa Mwanza, John Mongella pamoja akiwa ameambatana na viongozi
mbalimbali amekagua matayarisho ya ujenzi wa mnara, uzio na makaburi ya
baadhi ya abiria waliofariki kwenye ajali ya MV. Nyerere na kuzikwa
katika eneo la Bwisya kisiwani Ukara.
Baadhi
ya viongozi wa CCM wilayani Ukerewe wakiwaombea ndugu, jamaa na
marafiki waliopoteza majisha kwenye ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere
kilichokuwa kikitoka Kisiwa cha Bugolora kwenda Kisiwa cha Bwisya.
0 comments:
Post a Comment