Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye akiweka kizimia moto katika
moja ya vyumba vya madarasa katika shule inayotarajiwa kuwa shule ya
wanafunzi wenye vipaji vya michezo Simiyu Sekondari, wakati wa ziara
yake Mjini Bariadi Mkoani Simiyu, Juni 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka (kushoto) akimtambulisha Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye kwa baadhi ya wanafunzi wa
shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi kabla ya kuzungumza nao
juu ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto wakati wa ziara yake mkoani
Simiyu, Juni 19, 2019.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka wakiwasha moto kwa ajili ya kuwaonesha wananchi namna
ya kuzima moto pindi moto unapotokea, wakati wa ziara yake Mkoani
Simiyu, Juni 19, 2019.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye akizungumza na wanafunzi wa
baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mjini Bariadi, kuhusu
tahadhari na kinga dhidi ya majanga ya moto,wakati wa ziara yake Mkoani
Simiyu Juni 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka(kulia) akimuongoza Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini
Kamishina Jenerali Thobias Andengenye kukagua moja ya mabweni
yanayojengwa katika Shule ya Sekondari ya Simiyu, wakati alipotembelea
shule hiyo na kuzungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na
sekondari za Mjini Bariadi, kuhusu tahadhari na kinga dhidi ya majanga
ya moto,wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka(kulia) akimuongoza Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini
Kamishina Jenerali Thobias Andengenye kukagua moja ya mabweni
yanayojengwa katika Shule ya Sekondari ya Simiyu, wakati alipotembelea
shule hiyo na kuzungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi na
sekondari za Mjini Bariadi, kuhusu tahadhari na kinga dhidi ya majanga
ya moto,wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Askari wa jeshi la Zimamoto na uokoaji
mkoa wa Simiyu, akimuelekeza mmoja wa wanafunzi namna ya kuzima moto
wakati wa ziara ya Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kamishina
Jenerali Thobias Andengenye katika shule ya Sekondari Simiyu, wakati wa
ziara yake Mkoani Simiyu Juni 19, 2019.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye(katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mkoa wa
Simiyu wakati wa ziara yake Mkoani hapa Juni 19, 2019.
…………………
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
nchini Kamishina Jenerali Thobias Andengenye ameliagiza Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji, kuendelea kufanya ukaguzi wa kinga
na tahadhari ya moto kwa shule zote za sekondari za mabweni nchini
kujiridhisha ikiwa vigezo vimezingatiwa, kwa lengo la kuepusha majanga
ya moto yanayogharimu maisha ya watu na mali.
Andengenye ametoa maagizo hayo Juni 19,
2019 Mkoani Simiyu wakati akizungumza na wanafunzi wa baadhi ya shule
za msingi na sekondari za Mjini Bariadi katika shule ya sekondari
Simiyu, katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Akizungumza na wanafunzi Kamishina
Jenerali Thobias Andengenye amesema kumekuwa na matukio ya moto katika
shule kadhaa za bweni ambayo yameleta athari mbalimbali ikiwa ni pamoja
na kusababisha vifo kwa wanafunzi, kuteketea kwa mali, hivyo jeshi la
zimamoto na uokoaji linaendelea kuweka mikakati ya kukabiliana na
majanga hayo.
Amesema mikakati hiyo ni pamoja na
kusogeza huduma za zimamoto karibu na wananchi kufanya ukaguzi wa
tahadhari na kinga ya moto katika majengo, kusoma ramani za majengo na
kuanzisha klabu za zimamoto katika shule, ili kuwajengea wanafunzi uwezo
wa kujua vitu vya kufanya na vya kuepuka na uwezo wa kukabili moto
katika hatua za awali na kuuzima.
Katika hatua nyingine Andengenye
amewataka wamiliki wa shule kuzingatia ushauri wa kitaalam unaotolewa na
wataalam wakati wa ukaguzi juu ya namna ya kufanya mabweni , madarasa
na ofisi ziwe salama kwa kuwasilisha michoro ya majengo hayo katika
Ofisi za Zimamoto ili ushauri wa kitaalam uweze kutolewa.
“Niwaombe wanaomiliki shule wazingatie
ushauri wa kitaalam unaotolewa, wazingatie ujenzi unaofuata ushauri wa
kitaalaam kwa kuwasilisha michoro kama wanataka kujenga mabweni,
kuongeza madarasa au kuongeza vyumba vya ofisi basi wazingatie ushauri
ili majengo yanayojengwa yawe salama zaidi” alisema.
Aidha, amewaasa wananchi kuacha kuweka
mitungi ya gesi ndani na kutikisa mitungi ya gesi kama njia ya kufahamu
kiasi cha gesi kilichopo; kwa kuwa kunaweza kusababisha moto na kushauri
kuwa njia sahihi ya kupima kiasi cha gesi katika mtungi ni kuweka
mtungi katika maji, ambapo baada ya kuutoa sehemu isiyo na gesi
itaonekana kuwa kavu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka amesema kumekuwa na mwamko mkubwa wa watu kutumia gesi, hivyo
ameshauri Jeshi la Zimamoto na uokoaji kuendelea kutoa elimu katika
mikusanyiko ya watu na kupitia vyombo vya habari kuhusu dhana ya
matumizi sahihi ya gesi ili kuepusha majanga ya moto.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amelishukuru Jeshi la Zimamoto na uokoaji
kutoa elimu kwa wanafunzi na akawataka wanafunzi wote waliopata elimu
hiyo kuwa mabalozi katika maeneo yao wanayoishi.
Magreth Sonda mwanafunzi wa kidato cha
pili shule ya sekondari Simiyu ameshukuru kupata elimu ya tahadhari na
kinga dhidi ya moto na kuahidi kuwa yeye pamoja wanafunzi wenzake
watakuwa mabalozi wa kueneza elimu hiyo kwa jamii inayowazunguka ili
kuepusha majanga ya moto ambayo yana athari nyingi ikiwemo vifo na
kuteketea kwa mali.
0 comments:
Post a Comment