Ubalozi mdogo wa China ulipo Zanzibar umekabidhi msaada wa Chakula
na Vifaa mbalimbali kwa Watoto wanaoishi nyumba ya kulelea Watoto
Mazizini ikiwa ni mwendelezo wa kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia wa
muda mrefu katika ya Tanzania na Jamhuri ya watu wa China.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Mabegi ya Shule, Kalamu,
Madafatari, Mipira ya kuchezea, Maziwa, Sabuni na Manukato ili visaidie
kuwafariji Watoto hao kuelekea siku kuu ya Idd na maadhimisho ya siku ya
Mtoto wa Afrika.
Akikabidhi Msaada huo kwa niaba ya Ubalozi wa China Mke wa Balozi wa
China Mama Liu Jie amesema nchi rafiki wa China zimeongezeka duniani
lakini kamwe China haiwezi kuisahau Tanzania ambayo imekuwa rafiki wa
muda mrefu.
Amesema China itaendeleza uaminifu wake wa kisiasa na Tanzania na kushirikiana katika nyanja za kiuchumi na biashara.
Mama Lui ameongeza kuwa China itazidisha nguvu ya misaada kwa
Tanzania kwa lengo la kuwasaidia wananchi wake kuishi kwa furaha na
amani.
“Miaka ya 1970 ambapo uchumi wa China ulikuwa mdogo tuliweza
kusaidia kujenga Reli ya TAZARA, hivyo tutaendelea kusaidia mambo
mengine muhimu katika kipindi hiki ambapo uchumi wa China umekuwa na
kuwa Taifa la Pili duniani kiuchumi.” Alisema Mama Lui.
Kwa upande wake Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na
Watoto Moudline Cyrus Castiko ameishukuru China kwa kuendelea kuisadia
Tanzania katika Nyanja mbali mali za kimaendeleo.
Amesema Watoto ni nguvu kubwa ya kujenga Makabila na Taifa hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuwasaidia ili kutimiza malengo yao.
Amempongeza Mke wa Balozi huyo wa China kwa misaada mbali mbali
anayoitoa kwa Watoto ambapo mwaka 2017 akiwa na Mke wa Rais Shein
waliletea Vyakula, Vifaa vya kusomea na kupima afya za Watoto kituoni
hapo.
Waziri Castiko ametoa wito kwa jamii kutoa misaada ya mahitaji kwa
Watoto wanolelewa katika kituo hicho cha Mazizi ili kuwafariji.
“Kila mtu anahitaji kuguswa na watoto hawa ambao hawana Wazazi na
wito wangu anayetaka kuwasaidia aje kituoni ili awasaidie, kwa wale
wasio na uwezo hata kuwapa Mayatima hawa maneno ya faraja ni msaada
mkubwa kwao” aliongeza Mama Castiko.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa amesema kituo hicho cha kulelea Watoto
kwa sasa kina jumla ya Watoto 30 ambapo kati yao 16 ni Wasichana na 14
ni Wavulana.
Amesema Watoto hao wanahitaji kupendwa na kutiwa moyo ili
watakapokuwa watu wazima nao waweze kuwa na upendo wa kuihudumia wenzao
na nchi kwa ujumla.
Urafiki wa Jamhuri ya Watu wa China na Tanzania una historia ndefu
inayoimarishwa kila leo ambapo huu ni mwaka wa 55 tangu nchi hizo
zianzishe uhusiano wa kidiplomasia.
0 comments:
Post a Comment