Rais
Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha
kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Bi. Grace Hokororo kwa tuhuma za
kuingiza nchini raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya kuishi kinyume
cha taratibu.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya
kumaliza kikao na Makamishna wa uhamiaji. Kikao hicho kilifanyika Makao
Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
Pia
Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu
Nchemba kuunda tume ya uchunguzi kuhusu utoaji wa vibali uraia nchini.
Alisema haiwezekani raia wa kigeni wanaingizwa nchini na wanapewa vibali vya kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.
"Idara
ya Uhamiaji tunaitegemea kusimamia mipaka yetu na kuziba mianya ya watu
kuingia bila ya kufuata taratibu lakini kwa mapenzi yake Ofisa huyu
ameruhusu Wasomali kuingia bila kufuata taratibu." alisema Waziri Mkuu
Waziri Mkuu alisema ni lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini
"Tulidhani
ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa Wasomali hao ambao hawakuwepo
nchini wameingia na kupewa vibali moja kwa moja kwa mapenzi yake tu
sasa hii ni dosari hatuwezi kuivumilia. Hawa Wasomali aliowapa vibali
vya kuishi wala hawakuwa wanaishi nchini wameingia tu na kupewa vibali,
hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ameagiza ofisa huyo akae
pembeni na achunguzwe ni kujua ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa
raia hao" alisisitiza Majaliwa
0 comments:
Post a Comment