Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,
akizungumza wakati wa Majumuisho ya Semina ya Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Bajeti iliyohusu miradi ya umeme vijijini na
Kinyerezi 1 Extension, iliyofanyika jijini Dodoma. Kushoto kwa Naibu
Waziri ni, Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya
Nishati, Maseke Mabiki.
Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, REA na
TANESCO wakiwa kwenye Semina ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Bajeti iliyohusu miradi ya umeme vijijini na Kinyerezi 1 Extension,
iliyofanyika jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Bajeti, Viongozi wa Wizara ya Nishati, REA na TANESCO wakiwa kwenye
Semina iliyohusu miradi ya umeme vijijini na Kinyerezi 1 Extension,
iliyofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani,
akizungumza wakati wa Semina ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Bajeti iliyohusu miradi ya umeme vijijini na Kinyerezi 1 Extension,
iliyofanyika jijini Dodoma. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Bajeti, Viongozi wa Wizara ya Nishati, REA na TANESCO wakiwa kwenye
Semina iliyohusu miradi ya umeme vijijini na Kinyerezi 1 Extension,
iliyofanyika jijini Dodoma.
……………………
Na Teresia Mhagama, Dodoma
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
limetenga kiasi cha shilingi bilioni 400 kwa ajili ya kazi ya kusambaza
umeme kwenye maeneo takribani 754 yaliyopitiwa na miundombinu ya umeme
lakini hayana umeme.
Hayo yalisemwa tarehe 24 Juni, 2019
jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu wakati wa
Majumuisho ya Semina ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti
iliyohusu utekelelezaji wa miradi ya umeme vijijini na mradi wa
Kinyerezi 1 Extension (MW 185).
Semina hiyo ya siku moja ilihudhuriwa na
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati,
Dkt.Hamisi Mwinyimvua, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini
(REA), Wakili Julius Kalolo, Menejimenti ya Wizara ya Nishati, REA na
TANESCO.
“TANESCO imeshajipanga kufanya kazi hiyo
na Wizara inaendelea kusimamia kazi hizi za usambazaji umeme ili
kuhakikisha kuwa zinafanyika kwa ufanisi na tumeshafanya vikao mara
kadhaa ili na wadau wanaohusika na usambazaji umeme wakiwemo Mameneja wa
TANESCO nchi nzima lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata
umeme.” Alisema Naibu Waziri.
Aliongeza kuwa, katika mwaka wa Fedha
unaoanza mwezi wa Saba mwaka huu, kipaumbele kitakuwa ni usambazaji
umeme katika maeneo mbalimbali nchini kwani kila siku kuna ziada ya
umeme ya kiasi cha megawati 250 hadi 300 kwa siku.
Aidha kuhusu usambazaji umeme katika
Taasisi za umma kwenye miradi ya umeme vijijini alisema kuwa, Serikali
kupitia REA na TANESCO itaweka kipaumbele cha kupeleka umeme kwenye
maeneo hayo ili uwepo wa nishati kwenye vijiji hivyo uwe na tija.
Katika Semina hiyo, wajumbe hao
walielezwa mafanikio mbalimbali ya usambazaji umeme vijijini ambapo
ilielezwa kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Mei, 2019, jumla ya
Vijiji 7,217 kati ya Vijiji 12,268 ambayo ni asilimia 58.9 ya Vijiji
vyote vimefikiwa na miundombinu ya umeme.
Pia, hadi kufikia mwezi Juni 2020 jumla ya Vijiji 10,278 sawa na asilimia 84 ya Vijiji vyote vitakuwa vimepatiwa umeme.
Kuhusu utekelezaji wa mradi wa Kinyerezi I
Extension (MW 185) ilielezwa kuwa, mradi huo utakamilika mwezi Agosti
mwaka huu na mkandarasi ni kampuni ya Jacobsen Electro ya Norway.
Katika Semina hayo, Wajumbe hao walitoa
maoni mbalimbali yatakayoboresha Sekta ya Nishati nchini ambayo Wizara
ya Nishati kupitia Taasisi zake iliahidi kuyafanyia kazi.
0 comments:
Post a Comment