RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ameviagiza vyombo vya ulinzi
na usalama kuwakamata wale wote waliotaka kusafirisha karafuu nje ya
nchi kupitia bandari ndogo ya Kijiji cha Tondooni, Mkumbuu Wilaya ya
Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba hivi karibuni na kufikishwa mbele ya
vyombo vya sheria.
Akizungumza wakati alipotembelea Kituo Kikuu cha Karafuu cha Shirika
la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) Wete kukagua karafuu zilizokamatwa,
Dk Shein alisema uchunguzi ukifanywa kwa makini watu hao wanaofanya
biashara ya magendo watapatikana kwa kuwa wananchi wanawafahamu.
Taarifa ya Ofisa Mdhamini wa ZSTC, Pemba Abdullah Ussi ilieleza kuwa
Septemba 3, mwaka huu saa 11 alfajiri, askari wa Kikosi Maalumu cha
Kuzuia Magendo (KMKM) kilikamata viroba 17 vya karafuu kavu na vikonyo
viroba vinne.
Taarifa hiyo ilibainisha kuwa baada ya uchunguzi karafuu hiyo ilikuwa
imechanganywa na unga wa vikonyo uliosagwa pamoja na vipande, ambapo
baada ya kupimwa karafuu hiyo ilikuwa na uzito wa kilo 549, wakati unga
na uchafu mwingine, ulikuwa na uzito wa kilo 200.
Baada ya kuona uchafu huo uliochanganywa na karafuu hizo, Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alisema, vitendo hivyo ni
lazima vipigwe vita kwa nguvu zote kwa kuwa vinaharibu sifa ya karafuu
ya Zanzibar na alivitaka vyombo vya sheria kudhibiti hujuma hizo kwa
kutumia Sheria ya Karafuu Namba 11 ya mwaka 2011 ambayo imebainisha
adhabu dhidi ya watu hao.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Balozi Amina Salum Ali
alionesha kutoridhishwa na kasi ya hatua zinazochukuliwa dhidi ya watu
wanaoshukiwa kutenda uhalifu dhidi ya zao la karafuu.
Sunday, September 11, 2016
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Nimebahatika kupata fursa kadhaa kukaa na kuzungumza na Mheshimiwa Rais Mstaafu Hayati Benjamin William Mkapa enzi za uhai wake....
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya kilim...
-
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akizungumza na wachimbaji wadogo katika eneo la Mataba ndani ya Shamba la mit...
-
Na Mwandishi Wetu, Arusha Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Eng. Innocent Masaka, amesema wakala huo umejipanga kubore...
-
YANGA jana imerejesha furaha kwa mashabiki wake baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya Majimaji katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa kwenye...
Powered by Blogger.

0 comments:
Post a Comment