– Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo (kushoto) akimkabidhi
mkataba wa utekelezaji wa mradi wa Lishe Endelevu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Joachim Wangabo katika hafla ya uzinduzi wa Mradi huo uliofanyika
kitaifa mkoani Rukwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo (kushoto) akimkabidhi
mkataba wa utekelezaji wa mradi wa Lishe Endelevu Mkuu wa Mkoa wa
Iringa Ali Hapi katika hafla ya uzinduzi wa Mradi huo uliofanyika
kitaifa mkoani Rukwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo (katikati Mwenye
suti) katika picha ya pamoja na wakuu wa mikoa ya Songwe, Katavi, Iringa
na Rukwa pamoja na makatibu Tawala wa Iringa, Morogoro pamoja na
Waganga Wakuu wa mikoa ya Dodoma na Rukwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya
Sumbawanga muda mfupi baada ya uzinduzi wa kitaifa wa mradi wa Lishe
Endelevu.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim
Wangabo (wa pili toka kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ali Hapi (wa pili
toka kushoto) wakitia saini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa lishe
Endelevu unaodhaminiwa na Shirika la maendeleo la Watu wa Marekani
(USAID) muda mfupi kabla ya uzinduzi rasmi huku nyuma yao kukiwa na
makatibu tawala wa mikoa hiyo inayotekeleza mradi huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo (mwenye suti)
akiwasalimia wananchi walifika kupata huduma katika banda la Taasisi ya
Jakaya Kikwete kutoka kitengo cha Afya ya Moyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo (mwenye suti)
akiwatunza wanafunzi wa shule ya Sekondari Kizwite waliokuwa wakitoa
burudani ya wimbo wao wa Lishe Endelevu katika hafla ya uzinduzi wa
mradi wa lishe Endelevu uliofanyika kitaifa Mkoani Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi
(wa Kwanza kushoto) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera
wakikituza kikundi cha Kwaya cha Laela kilichokuwa kikitoa burudani
katika viwanja Ndua Mjini Sumbawanga kulifanyika hafla ya uzinduzi wa
kitaifa wa mradi wa Lishe Endelevu.
…………………
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo amewaagiza wakuu wa
Mikoa minne iliyopo kwenye mradi wa “lishe Endelevu” kuhakikisha kuwa
mikataba hiyo ya utekelezaji wa afua za lishe inawashukie wakuu wa
Wilaya, nao wasainiane na wakurugenzi wa halmashauri, nao pia waishushe
kwa watendaji wa kata na watendaji hao wasainiane na watendjai wa vijiji
na mitaa ili utekelezaji wa mikataba hiyo kuwa shirikishi bila ya
kubagua eneo lolote la utawala.
Amesema kuwa pamoja na utekelezaji
wa mradi huo, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa niaba ya Makamu
wa Rais alisainishana mkataba wa utekelezaji wa afua za lishe na wakuu
wa Mikoa yote nchini ili kuchochea utekelezaji wa shughuli za lishe hapa
nchini, mkataba ambao una viashiria kumi ambavyo vinampima Mkuu wa Mkoa
kila baada ya miezi sita na utadumu kwa kipini cha miaka minne kuanzia
januari 2018 hadi 2021
“Kwa vile eneo hili ni eneo la
mradi maalum, nitatamani sana niweze kuona katika mbao za vijiji vyetu
ambavyo miradi hii inatekelezeka, tuwe na taarifa licha ya taarifa ya
mapato na matumizi, kuwe na taarifa ambayo inasema katika Kijiji X,
Kijiji cha Milepa, Kijiji cha Wampembe ama Kijiji kingine inaonesha
watoto wenye udumavu ni wangapi na watoto wenye upungufu wa damu ni
wangapi, hili jambo ninlazima tushikane kila mtu atomize wajibu wake
kuhakikisha ajenda ya lishe tunaisimamia kwa nguvu zote,” Alisisitiza.
Ameyasema hayo alipokuwa akizindua
mradi wa Lishe Endelevu unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Watu
wa Marekani (USAID) unaotekelezwa katika Mikoa minne ya Iringa, Dodoma,
Morogoro pamoja na Rukwa ikiwa ni mchango wa Serikali ya Marekani katika
kuisaidia Serikali ya Tanzania kufikia lengo la kupunguza tatizo la
udumavu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano kutoka asilimia 34 hadi
asilimia 28 ifikapo mwaka 2021.
Akitoa salamu za mkoa, Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo alitaja baadhi ya mambo yanayopelekea
wananchi wa Mkoa wa Rukwa, hususan watoto wenye umri wa chini ya miaka
mitano kuwa na hali duni ya lishe huku akisistiza Utamaduni na mazoea ya
wananchi wengi kutumia aina fulani za vyakula hususan nafaka kwa muda
mrefu bila kuchanganya na makundi mengine ya vyakula, hivyo kukosa
virutubishi muhimu.
“Wananchi wengi hasa wanaoishi
Vijijini kutokuwa na Elimu ya kutosha kuhusu masuala ya lishe
bora.Baadhi ya akinamama na familia kwa ujumla, kutozingatia taratibu za
unyonyeshaji na ulishaji bora kwa watoto wenye umri chini ya miaka
miwili. Baadhi ya akina mama wenye watoto wadogo kukosa muda wa kutosha
wa kuwahudumia watoto wao kwa lishe bora,” Alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Shirila la Maendeleo la Watu wa Marekani Andrew Karas aliishukuru
serikali kwa kuweka kipaumbele juhudi za kuhakikisha inapunguza hali ya
udumavu nchini kwa kutekeleza afua mbalimbali kuanzia ngazi ya kitaifa
hadi kwenye halmashauri huku akimpongeza mgeni rasmi wa shughuli hiyo
Suleima Jafo na Wizara ya TAMISEMI kwa kutoa kipaumbele maboresho ya
lishe.
“Sisi sote tunatambua mchango wa
Lishe katika maendeleo jumuishia na maendeleo endelevu, tunavyojua
Tanzania inaendelea kukumbwa na viwango vya juu vyua utapiamlo Mkoani
Rukwa zaidi ya nusu ya watoto waliochini ya miaka mitano wana udumavu
ambayo ni asilimia kubwa zaidi nchini, utapiamlo una athari mbaya kwa
mtu binafsi, familia na taifa, unaathiri maendeleo ya Kimwili na pia
kiakili, lishe duni huchangia kuwa na uwezo mdogo wa kujifunza,”
Alisema.
Mradi huu unalenga kuongeza na
kuboresha upatikanaji na utoaji wa huduma bora za lishe katika vituo vya
afya na jamii, uzalishaji na ulaji wa vyakula vyenye virutubishi kwa
wingi katika ngazi ya kaya, udhibiti wa usawa wa kijinsia katika mapato
na matumizi ya rasilimali za nyumbani ili kuhakikisha upatikanaji wa
vyakula mchanganyiko.
Shirika la maendeleo la Watu wa
marekani limetenga zaidi ya dola za kimarekani milioni 19 ili kutekeleza
mtadi wa lishe Endelevu kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2018
hadi 2022 katika Mikoa minne na Halmashauri 22 za Tanzania Bara na
kulenga kufikia zaidi ya wanawake milioni 1.5 walio katika umri wa
kuzaa, watoto milioni 1.1 walio chini ya umri wa miaka mitano na vijana
walio katika rika la baleghe 330,000 wenye umri wa miaka 15-19.
0 comments:
Post a Comment