*************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Juventus ya nchini
Italia imemtangaza aliyekuwa kocha wa klabu ya Chelsea Maurizio Sarri
kuwa kocha wao mpya atakaeiongoza klabu hiyo kwa msimu ujao.
Muitaliano huyo amejiunga na
Juventus kwa mkataba wa miaka mitatu akichukua mikoba ya Massimiliano
Allegri ambaye alitangaza kutundika daruga hivi karibuni.
Ikumbukwe kuwa kocha huyo
ameiongoza klabu ya Chelsea kwa msimu mmoja na kuisaidia kunyakuwa taji
la Ueropa league mbele ya mahasimu wao wa jiji moja Arsenal na pia
kuisaidia klabu hiyo kushiriki michuano ya klabu Bingwa Ulaya kwa msimu
ujao.
Chelsea watapata fidia ya £5M
kutoka Juventus kutokana na dili hilo ambalo huenda likafungua milango
kwa Frank Lampard kujiunga na Chelsea kama kocha mkuu.
0 comments:
Post a Comment