Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na
TANESCO wakiwa katika kikao baina ya Wizara ya Nishati, TANESCO na REA
kilichofanyika jijini Dodoma na kuongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt.
Medard Kalemani.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,
akizungumza wakati wakati wa kikao baina ya Wizara ya Nishati, TANESCO
na REA kilichofanyika jijini Dodoma na kuongozwa na Waziri wa Nishati,
Dkt. Medard Kalemani.
Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na
TANESCO wakiwa katika kikao baina ya Wizara ya Nishati, TANESCO na REA
kilichofanyika jijini Dodoma na kuongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt.
Medard Kalemani.
Watendaji kutoka Wizara ya Nishati,
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na TANESCO wakiwa katika kikao baina ya
Wizara ya Nishati, TANESCO na REA kilichofanyika jijini Dodoma na
kuongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt
Hamisi Mwinyimvua akizungumza katika kikao baina ya Wizara ya Nishati,
TANESCO na REA kilichofanyika jijini Dodoma na kuongozwa na Waziri wa
Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
Watendaji kutoka Wizara ya Nishati,
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na TANESCO wakiwa katika kikao baina ya
Wizara ya Nishati, TANESCO na REA kilichofanyika jijini Dodoma na
kuongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani
akizungumza katika kikao baina ya Wizara ya Nishati, TANESCO na REA
kilichofanyika jijini Dodoma.
…………………..
Ili kuhakikisha kuwa kazi ya usambazaji
umeme mijini na vijijini inafanyika kwa kasi na ufanisi katika mwaka wa
fedha 2019/20, viongozi wa Wizara ya Nishati wakiongozwa na Waziri wa
Nishati, Dkt Medard Kalemani wamefanya Mkutano wa siku moja na watendaji
wa TANESCO na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ili kujadili masuala
mbalimbali yatakayowezesha lengo hilo linafanikiwa.
Mkutano huo, uliofanyika tarehe 16 Juni,
2019, ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu
Mkuu, Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Menejimenti ya TANESCO,
REA na Bodi ya REA, ulijadili kazi zilizofanyika katika mwaka 2018/19
na kujipanga katika utekelezaji wa majukumu kwa mwaka wa fedha wa
2019/20 unaoanza mwezi Julai.
Baadhi ya masuala yaliyojadiliwa kwenye
kikao hicho ni upelekaji umeme viwandani, kuimarisha hali ya umeme
katika maeneo yaliyounganishwa na gridi, kuunganishia umeme Taasisi za
umma, kuunganishia umeme maeneo yaliyopitiwa na miundombinu ya umeme,
bei ya kupeleka umeme vijijini, ununuzi vifaa vya umeme, utambuzi wa
wateja wanaohitaji umeme viwandani na utambuzi wa wazalishaji wadogo wa
umeme.
“ Kimsingi lazima tuhakikishe
tunaimarisha huduma za umeme kwa kutatua kero mbalimbali kama za
kukatika kwa umeme na kutowaunganishia umeme wateja ndani ya muda
uliopangwa hivyo lazima tujipange sasa kukamilisha shughuli zetu kwa
ukamilifu ili kuwezesha nchi kuingia kwenye uchumi wa viwanda.” Alisema
Dkt Kalemani
Suala la upelekaji umeme viwandani,
Waziri wa Nishati, amesema kuwa ni la kipaumbele na ametoa miezi mitatu
kwa Mameneja wa TANESCO wa Wilaya kuwasilisha takwimu ya viwanda
walivyoviunganishia umeme kwenye maeneo yao.
Aidha, amewaagiza kuhakikisha kuwa,
wanafanya jitihada za kuunganishia umeme viwanda vinavyoanzishwa kwenye
maeneo yao kabla havijakamilika kwa kupeleka bili stahiki kwa wenye
viwanda ili waweze kufanya malipo mapema hivyo TANESCO kutoonekana kuwa
ni chanzo cha kukwamisha ufanyaji kazi wa kiwanda.
Kuhusu upelekaji umeme vijijini, Dkt
Kalemani amesema kuwa kila mtumishi wa Wizara, TANESCO na REA lazima
atambue kuwa, lengo la Serikali ni kupeleka umeme katika Vijiji vyote
ifikapo Juni 2021 hivyo ni lazima kila mmoja ahakikishe kuwa hilo
linafanikiwa na bei ya kuunganisha umeme ni 27,000 na Meneja asiyetaka
kutekeleza hilo aachie ngazi.
Aidha, kuhusu Wazalishaji wadogo wa umeme
ameelekeza Mameneja wa TANESCO wilayani kuhakikisha kuwa, wanawatambua
wazalishaji hao, wanawapa elimu, miongozo, wanawasimamia na kuwaingiza
katika programu za uzalishaji umeme.
Suala jingine lililojadiliwa ni ununuzi
wa vifaa vya umeme, ambapo Dkt Kalemani amesema kuwa mtendaji anapaswa
kusimamia utekelezaji wa agizo la Serikali la kutonunua nje vifaa vya
umeme vinavyopatikana nchini ili kurahisisha ufuatiliaji wa vifaa hivyo
pia kuokoa muda mrefu ambao ungetumika kusafirisha vifaa hivyo kutoka
nje ya nchi.
Suala la uunganishaji umeme kwa wateja wa
muda mrefu pia lilijadiliwa ambapo Waziri wa Nishati ametoa mwezi mmoja
kwa TANESCO kuunganishia umeme wateja wote waliolipia umeme kwa muda
mrefu na bado hawajaunganishwa na umeme.
Kazi ya kushusha umeme kwenye maeneo
yaliyopitiwa na miundombinu ya umeme ameagiza kuwa, kazi hiyo ianze
mwezi wa Saba mwaka huu na ikamilike ndani ya miezi Sita.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati,
Subira Mgalu amesisitiza kuhusu upelekaji umeme kwenye Taasisi za umma
kama vile Shule, Zahanati na Visima vya Maji kutokana na umuhimu wake
kwa jamii zinazozunguka maeneo hayo na kuagiza kuwa suala hilo liwekewe
mkakati maalum.
Vilevile amempongeza Waziri wa Nishati
kwa kuwa na utaratibu wa vikao kazi ambavyo vimekuwa na tija katika
uendelezaji wa Sekta ya Nishati nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt
Hamisi Mwinyimvua amempongeza Waziri wa Nishati kwa Mkutano huo na
kuahidi kuwa changamoto mbalimbali zilizojadiliwa kwenye Mkutano
zitafanyiwa kazi.
Aidha, amegiza watendaji wa Taasisi
zilizohudhuria Mkutano huo kutekeleza ipasavyo maagizo yaliyotolewa na
Waziri wa Nishati na kuendelea kufanya kazi kwa bidii.
Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati
Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga amemshukuru Waziri wa Nishati kwa
kufanya Mkutano huo ambao unasaidia kuboresha utendaji kazi na kutoa
wito kwa TANESCO kuendelea kutatua changamoto mbalimbali kama za
kukatika umeme na kutounganishia umeme wateja ndani ya muda mfupi.
0 comments:
Post a Comment