Mkuu wa mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo
ametoa ushauri kwa wadau wa michezo nchini kuona namna ya kuimarisha
mbinu za kuibua vipaji vya wanamichezo kuanzia ngazi ya shule za msingi
katika mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA ili kuweza kuwa na vijana
watakaoweza kubeba jina la Tanzania katika michezo.
Amesema kuwa yeye ni miongoni mwa watu
waliochelewa kulala ili kuangalia mechi baina Tanzania maarufu kama
Taifa Starts na jirani zetu Kenya maarufu kama Harambee Strars ambapo
hadi kumalizika kwa mchezo huo Harambee Stars iliibuka kidedea kwa
kuilaza Taifa Stars mabao 3 kwa 2.
“Kuna ambao wamelala alfajiri na wengine
wapo humu ambao wamelala leo, tunaomboleza kufungwa huku, tungeshinda
jana tungekuwa na mwanga wa kusonga mbele, sasa ni kinyume na
yalivyokuwa matarajio yetu lakini ndugu wana Rukwa tusikate tamaa,
tuendelee kuiunga mkono timu yetu hii ya Taifa, Kufungwa ni kujifunza,
tuendelee kujipanga vizuri hasa kwa vijana kuanzia UMISHAMTA huku mpaka
UMISETA na kwenye “academy” hizi,” alieleza.
Aidha, alibainisha kasoro kadhaa
zinazojitokeza katika ligi yetu ya Tanzania hasa kwa upande wa timu
vinara zinazopata nafasi za kwenda kucheza makombe ya Kalbu Bingwa
Afrika pamoja na Kombe la Shirikisho kuona namna ya kutoa fursa kwa
wachezaji wa kitanzania ili wapate ujuzi wa kimataifa na sio kuwajenga
wachezaji wa nje ambao wanakwenda kutumikia nchi zao.
“Hizi timu zetu za Yanga na Simba pamoja
na Azama zinafanya vizuri kwasababu zina wachezaji wengi wa kigeni
matokeo yake timu ya Taifa inapokwenda kwenye mashindano wachezaji wetu
wanabaki wenyewe, angalieni Emanuel Okwi anavuma kule Uganda lakini
tumemuwezesha sisi hapa Tanzania,” Alisema.
0 comments:
Post a Comment