Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini,
Diana Madukwa,akisoma taarifa kwa Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mstaafu
Mizengo Pinda wakati akifungua mafunzo ya ujasiliamali kwa wanafunzi wa
vyuo vikuu vilivyopo mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania
(UWT) Wilaya ya Dodoma Mjini, Winifrida Kaliyo,akizungumza na wasomi
kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda
wakati alipofungua mafunzo ya ujasiliamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu
vilivyopo mkoani Dodoma
Baadhi ya wasomi wakifuatilia hotuba ya
mgeni rasmi Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda wakati akifungua mafunzo
ya ujasiliamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Dodoma
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda
akipokea Taarifa kutoka kwa Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana
Madukwa kabla ya kufungua mafunzo ya ujasiliamali kwa wanafunzi wa vyuo
vikuu vilivyopo mkoani Dodoma
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo
Pinda,akizungumza na wasomi nchi wakati wa kufungua mafunzo ya
ujasiliamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Dodoma
……………..
Na.Alex Mathias,Dodoma
WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ameweka
mambo muhimu tano ya kuzingatia kwa wasomi wa vyuo vikuu yatakuwa
msaada kwao kuelekea zuala nzima la ukosefu wa ajira nchini.
Hayo ameyasema leo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya ujasiliamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Dodoma.
Mhe.Pinda amewaambia kuwa serikali
haiwezi kuwaajiri vijana wote wanaohitimu elimu ya juu hivyo amewataka
wawe na njia ya pili ambayo itawapa mtaji.
“Nchi haiwezi kuajiri wasomi wote ili
niliweke wazi hivyo tulipaswa kutengeneza mfumo ambao utawafanya
wahitimu kuwa na muelekeo wa kutumia fursa zilizopo”amesema Mhe.Pinda
Mhe.Pinda ametaja jambo la kwanza ni
kuwepo kwa mfumo wa elimu utakaowawezesha kupata elimu ya ujasiliamali
katika kila ngazi ya masomo wanayoifikia.
“Kama mwaka wa kwanza hadi mwaka wa tatu
kwenye masomo yake akapatiwa mbinu mbalimbali zitakazomuwezesha kubaini
fursa za ujasiliamali zilizopo, kwa kiasi kikubwa tutaweza kukabiliana
na ukosefu wa ajira”aamesema Pinda
jambo la pili amewataka wasomi kuzingatia ni kubadili mtizamo wa kifikra kwamba pindi watakapo hitimu masomo wataajiriwa.
Aidha amesema kuwa alifanya ziara ya
kuongea na wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo mmoja wa wasomi
wa masomo ya sheria,alimueleza jinsi alivyopata tabu pindi alipoambiwa
afuge kuku, wakati amejifunza masuala ya sheria.
Jambo la tatu ambayo wanafunzi hao ni muhimu kuzingatia ni kufahamu uhalisia wa dunia ya sasa.
“Itawalazimu mshindane na watu kutoka
mataifa mengine ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) au maeneo mengine
duniani”amesisitiza
Pinda ametaja jambo la nne ambalo ni uthubutu katika kufanya maamuzi.
Amesema kuwa baadhi ya wasomi wa vyuo vikuu wamekuwa na desturi ya kuwakatisha tamaa wenzao ambao wana mawazo ya kujiajiri.
Mhe.Pinda amemalizia jambo la tano ambalo
amewaeleza wanafunzi hao ni kufahamu tofauti waliyokuwa nayo na wale
ambao hawakupata fursa ya kusoma elimu ya juu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa
Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Dodoma Mjini, Winifrida Kaliyo,
amesema kuwa semina hiyo imelenga kuwawezesha wanafunzi kutambua fursa
kisha kuzitumia kiuchumi.
Awali Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma
Mjini, Diana Madukwa, amesema kuwa tangu Januari hadi Juni mwaka huu,
umoja huo umeongeza wanachama wapya 1500.
Aidha,amesema kuwa wametoa mafunzo kwa
viongozi ngazi ya kata hadi wilaya pamoja na kuhamasisha wanawake
kugombea ngazi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
0 comments:
Post a Comment