Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Dkt. Hamisi Kigwangalla akifungua hafla ya utoaji wa Tuzo za
Waongoza Watalii nchini (Tanzania Tour Guides Awards 2019) kwa mwaka
,jijini Arusha.
Waziri wa Maliasili na
Utalii,Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi tuzo ya Mwongoza Watalii
Bora upande wa Wanaume, Bw. Athuman Njiku, wakati wa hafla ya utoaji wa
tuzo kwa waongoza watalii jijini Arusha
Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Tuzo ya mwongoza
Watalii Bora wa muda mrefu Bi. Mary Mushi kwa kufanya kazi ya kuongoza
Watalii Mlima Kilimanjaro tangu mwaka 1979.
Mjumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Mwenyekiti wa Kamati
hiyo kwa upande wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe. Peter Msigwa,
kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla
akikabidhi tuzo kwa mshindi wa Waongoza Watalii Bora wa muda mrefu kwa
upande wa wanaume.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Kemilembe Walter
akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo
kwa waongoza watalii kwa mwaka 2019, jijini Arusha
Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Kemilembe Walter
akimkabidhi Tuzo ya Mwongoza Watalii Bora kwa upande wa Wanawake mwaka
2019, Rehema Otalu wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo hizo jijini
Arusha.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi Tuzo kwa Niaba
ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla mmoja wa
waashindi wa Tuzo ya waongoza Utalii Bora upande wa Utamaduni kwa mwaka
2019, jijini Arusha.
Mjumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili, Utalii na Mbunge wa Nungwi –
Zanzibar, Mhe. Yusuf Haji Khamis kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na
Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla, akimkabidhi Tuzo ya Mwongoza Watalii
Bora Bw. Gaudence Phesto kutoka kampuni ya Kuongoza watalii ya Leopord
aliyeweka rekodi ya kupanda na kushuka Mlima Kilimanjaro kwa kutumia
muda wa saa 8.
Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiwapongeza Washindi wa
Tuzo ya Waongoza Watalii Bora kwa mwaka 2019 kwa upande wa Wapagazi
Wanawake. Wa pili kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa mashindano ya Tuzo hizo
Bw. Mozes Njowe kutoka Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori MWEKA.
Majaji walioshiriki
kuteua washindi wa Tuzo za waongoza Watalii kwa mwaka 2019 wakiwa
katika picha ya pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili
na Utalii na Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada ya
utoaji wa tuzo hizo jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Kemilembe Walter akimkabidhi Bi.
Alisya Sanga Tuzo ya Mwongoza Watalii Bora kwa niaba ya Waziri wa
Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa hafla ya Utoaji wa
Tuzo kwa Mwongoza watalii Bora wanawake mwaka 2019, jijini Arusha.
0 comments:
Post a Comment