Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa
akikagua pampu mpya ya maji iliyofungwa katika kijiji cha Mpapula
Halmashauri ya Wilaya Mtwara mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa
ziara ya kikazi kukagua miradi ya maji.
Waziri Mbarawa akielekea eneo ilikofungwa
pampu mpya ya maji katika kijiji cha Mpapula mkoani Mtwara ambapo
huduma ya maji imerejea baada ya pampu hiyo kuungua kwa muda na
alipofika Waziri wa Maji mwaka jana aliagiza pampu mpya inunuliwe haraka
ili wananchi wapate majisafi na salama.
……………………..
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame
Mbarawa (Mb) ameridhishwa na kurejea kwa huduma ya maji katika kijiji
cha Mpapula kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara baada ya
wananchi hao kufungiwa pampu mpya na kuanza kufanya kazi.
Waziri aliyasema hayo leo mara baada ya
kufika katika kijiji cha Mpapula na kukuta pampu ya maji mpya
iliyofungwa inafanya kazi baada ya pampu ya zamani kuungua mwaka jana.
Pampu hiyo iiliharibika mwaka jana na
haikuwa katika sehemu ya Mkataba wa Mkandarasi hivyo kupelekea wananchi
kukaa kwa muda mrefu bila ya kupata majisafi na salama hadi Waziri wa
Maji alipokuja kujionea tatizo hilo na kuahidi kuwanunulia pampu.
“Serikali iliahidi na imetekeleza”
alisema Waziri Mbarawa wakati akikagua pampu hiyo. Mradi huo wa Mpapula
unahudumia kata 2 ya Mpapula na muungano na wananchi wapatao 5953
wananufaika na mradi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi
Mmanda alisema kununuliwa kwa pampu hiyo kutasaidia kuondoa kilio cha
shida ya maji kwa wananchi wa kijiji cha Mpapula, na kuwataka wananchi
wa eneo hilo kutochimba katika njia ambazo mabomba yanapita. Kufanya
hivyo kutasaidia kutunza mabomba hayo yasipasuke na kufanya huduma ya
maji kuwa endelevu kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment