Naibu
Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt.Dorothy
Gwajima akizungumza katika kikao cha wadau wa Afya kilichofanyika katika
ukumbi wa Takwimu Jijini Dodoma.\Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt.
Zainabu Chaula akizungumza katika kikao cha wadau wa Afya Kilichofanyika
katika Ukumbi wa Takwimu Jijini Dodoma.Wadau wa Afya wakifuatilia kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Takwimu Jijini Dodoma.
…………………….
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Dorothy Gwajima
amewataka wadau wote wanaotoa huduma Tembezi za Afya kuunganisha nguvu
kwa pamoja ili huduma hiyo iweze kufikishwa katika Halmashauri zote
Nchini.
Dkt.Gwajima ameyasema hayo wakati wa
kikao cha wadau wa Afya kuwasilisha Taarifa mbalimbali za utekelezaji wa
miradi kilichofanyika katika Ukumbi wa Takwimu Jijini Dodoma.
Akizungumza katika kikao hicho Dkt. Gwajima
amesema huduma Tembezi za Afya ni muhimu kufikishwa katika Ngazi ya
Jamii ili wananchi waweze kupata matibabu kutoka kwa madaktari bingwa
tena kwa gharama nafuu.
“Huduma hizi zimekuwa zikitolewa na
Taasisi tofauti kwa nyakati tofauti na kila Taasisi analenga eneo Fulani
ambalo anachagua hivyo kuna maeneo ambayo yamekuwa yakinufaika na
huduma hizi mara kwa mara lakini kuna sehemu nyingine hazifikiwi kabisa
sasa ni umefika wakati wa kukaa pamoja na kuunganisha nguvu ya wadau
wote pamoja na Serikali na kupelekwa huduma hii katika Halmashauri zote
ili kila mwananchi mwenye uhitaji anufaike nayo”
Kupitia Kikao hiki cha leo tutaunda
Kamati ya Uendeshaji ambayo itahusisha Wataalamu wa OR-TAMISEMI, Wizara
ya Afya, Asassi zisizo za Kiserikali pamoja na wadau wanaotekeleza Afua
za Afya ambao watakuja na hadidu za rejea zitakazotuongoza katika
kutekeleza azima yetu hii kwa ufanisi aliongeza Dkt.Gwajima.
Pia Dkt. Gwajima alisema kuwa “Tunajua
tuna vituo vya kutolea huduma vya lakini si wakati wote vituo hivyo
vinakuwa na madaktari Bingwa na kwa mwananchi wa kawaidia kusafiri mpaka
kukutana na madaktari bingwa ni gharama hivyo tukisogeza huduma hizi
tutawatibu wananchi wetu hata yale magonjwa ambayo walikuwa wameyakatia
tamaa”Alisema Dkt. Gwajima.
Dkt. Gwajima aliongeza kuwa Huduma
hizi Tembezi zina faida zake kwanza gharama za kuwekeza katika huduma
hii ni ndogo lakini inawafikia watu wengi tena kwa muda mfupi. Unafuu
huu wa gharama sio kwa sisi kama watoa huduma lakini pia kwa wagonjwa
ambao ndio wanufaika wa huduma hii yaani ugonjwa ambao angeweza kutumia
zaidi ya shilingi milioni moja anaweza kupata huduma hiyo hiyo kupitia
Kliniki Tembezi kwa elfu thelathini tu.
“Huduma tembezi ni msaada kwa wanyonge,
wananchi wanaugua magonjwa makubwa ambayo hata akisafiri kumfuata
Daktari Bingwa anaweza akafia njiani kabla hata hajakutana na huyo
Daktari, kupitia huduma hii watakutanishwa na Madaktari bingwa kwa
urahisi na nafuu zaidi na hapo tutakuwa tumegusa maisha ya watanzania na
kuwaongezea siku za kuishi maana wangeweza kufa kwa kukosa huduma za
Afya stahiki kwa magonjwa yanayowasumbua” Alisema Dkt. Gwajima.
Tusipowafuata na kuwatibu wananchi
wataendelea kunywa miti shamba na kwenda kwa waganga na hata wakati
mwingine kupoteza maisha yao kwa kukosa matibabu stahiki hebu tuwafikie
wote kupitia huduma hii ya Kliniki Tembezi alimalizia Dkt. Gwajima.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainabu Chaula
amesema agenda kuu katika Sekta la Afya ni Huduma ya Afya kwa Wote na
hakuna mtu atakayeachwa nyuma hivyo ni lazima tuifikishe huduma hii ya
Kliniki Tembezi kwa wananchi wote.
“Tunapoelekea katika Uchumi wa Kati ni
wajibu wetu kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na Afya Njema ili aweze
kushiriki kikamilifu katika kujitafutia kipato sasa hii kazi kwetu
itakua rahisi tukiunganisha nguvu na rasilimali katika kutoa huduma hii
ya Afya Tembezi tushirikiane kikamilifu kuleta tabasamu kwa watanzania”
Alisema Dkt. Chaula.
Akiwasilisha Taarifa ya Huduma za Afya Tembezi Mratibu wa Huduma hiyo Dkt. Mombeki Domisian
amesema tangu walipoanza kutoa huduma hii katika Mkoa wa Singida
imeokoa maisha ya watanzania, imetoa elimu ya Kinga, imepeleka utaalamu
na zaidi imetoa ushauri kwa wagonjwa kulingana na ugonjwa husika.
0 comments:
Post a Comment