Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisikiliza maelezo kutoka
kwa Meneja Biashara kutoka Shirika la AFRIpads Bi. Liz McNeil wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani jijini Dodoma.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akishika Taulo ya kike
kuangalia ubora wake katika maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani
jijini Dodoma kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mak’s Ama Home
Pharmacy.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisoma jarida la Fema wakati
alipotembelea katika Banda lao katika maadhimisho ya Siku ya Hedhi
Salama Duniani jijini Dodoma kushoto ni Msaidizi wa Masuala ya Kihabari
kutoka Shirika la Femina Hip Bi. Sekela Mwaipaja.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa na wadau wa hedhi
Salama wakati wa maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani jijini
Dodoma.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika
Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya wadau wa Hedhi Salama
nchini wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya
Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.
*********************************************
Na.WAMJW-Dodoma
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameahidi kuweka masuala ya
hedhi salama kwenye Sera mpya ya Afya ambayo iko mbioni kukamilika ili
kuona kama hedhi salama imewekwa kama kipaumbele.
Ameyasema hayo leo jijini Dodoma
wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani ambayo
kitaifa yamefanyika jijini hapa.
Waziri Ummy amesema masuala ya
hedhi salama katika jamii hususan watoto wasichana na wanawake ni muhimu
katika kuweka hali ya usafi wa mazingira rafiki ambapo katika nchi
zinazoendelea ikiwemo Tanzania inakabiliwa na changamoto za upatikanaji
wa maji safi na salama, vyoo bora hasa mashuleni na sehemu za kazi
vyenye chumba cha kubadilishia wakati wa hedhi.
“Katika ripoti za UNICEF na WHO ya
mwaka 2013 zinasema kuwa katika kila msichana mmoja kati ya kumi
kusini mwa jangwa la sahara anakosa kwenda shule kwa siku tatu hadi tano
kwa sababu ya kuwa kwenye siku za hedhi”,Alisema Waziri Ummy.
Hata hivyo alisema asilimia 52 ya
vyoo vya wasichana mashuleni havina milango na ni asilimia 1 tu ya shule
zimetenga chumba maalum kwa ajili ya wasichana kujisitiri wakiwa kwenye
hedhi kikiwa na maji na vifaa vya hedhi.
Aidha, aliwataka wadau kuweka
mkazo kwenye kuongeza uelewa kwa wafanyabiashara kuzingatia upunguzaji
wa bei kwani taulo za hedhi si bidhaa ya anasa ila ni bidhaa muhimu kwa
mstakabali wa afya na maendeleo ya wanawake na wasichana nchini.
Waziri Ummy ametoa rai kwa wadau
wote wa hedhi salama kutenga fedha kwa ajili ya kujenga walau choo
kimoja cha mfano katika halmashauri kwani jamii ipo tayari kuchangia
maendeleo. Aidha, amekusudia kila taulo za kike zikatazoingizwa au
kuzalishwa Tanzania ziwe na idadi maalumu za katika kila paketi angalau
taulo kumi.
0 comments:
Post a Comment