Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akipokewa na Rais wa Chama Cha
Maafisa Uhusiano wa Sekta Binafsi Tanzania (PRST) Loth Makuza, mara
baada ya kuwasili katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam leo
Ijumaa (Mei 24, 2019) kwa ajili ya kushiriki katika Kilele cha
Maadhimisho ya Wiki ya Mawasiliano Barani Afrika. Kushoto ni Mratibu
Mwenyekiti wa Bodi ya (PRST), Jossey Mwakasyuka.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na
wadau mbalimbali wa sekta ya habari na Mawasilino kutoka Taasisi za
Umma na sekta binafsi wakati wa kilele cha maadhimisho ya ya Wiki ya
Mawasiliano Barani Afrika iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini
Dar es Salaam leo Ijumaa (Mei 24, 2019).
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo,. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wadau
mbalimbali wa sekta ya habari na Mawasilino kutoka Taasisi za Umma na
sekta binafsi wakati wa kilele cha maadhimisho ya ya Wiki ya Mawasiliano
Barani Afrika iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es
Salaam leo Ijumaa (Mei 24, 2019).
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja
na wadau mbalimbali wa sekta ya Habari na Mawasiliano pamoja na
wadhamini wa Maadhimisho ya Wiki ya Wiki ya Mawasiliano Barani Afrika
wakati wa kilele cha maadhimisho hayo yaliyofanyika leo Ijumaa (Mei 24,
2019).
Waziri wa Habari, UItamaduni,
Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akibadilishana
mawazo na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (katikati)
mara baada ya kufunga maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Mawasiliano
Afrika yaliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam leo
Ijumaa (Mei 24, 2019). Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO)
na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi.
(PICHA NA MAELEZO)
………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu,
MAELEZO-DAR ES SALAAA
WAZIRI wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amevitaka vyombo ya habari vya
Nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania kutangaza na kuandika habari za
kweli ili kujitofautisha na vyombo vya Nje ya Bara hilo ambavyo
upotosha na kubeza kwa makusudi mambo mazuri yanayotekelezwa na
yaliyotekelezwa na Nchi za Afrika.
Akizungumza katika kilele cha
Maadhimisho ya Wiki ya Mawasiliano Barani Afrika leo Ijumaa (Mei 24,
2019) Jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwakyembe alisema vyombo vya Habari vya
Afrika havina budi kuonyesha udhubuti kwa kuweka sera zinazoakisi
maendeleo na kuyatangaza kwa Wananchi wake na wote waliopo nje ya Bara
hilo.
Dkt. Mwakyembe alisema sehemu
kubwa ya maudhui ya Vyombo vya Habari vilivyopo nje ya Bara la Afrika
vinavyoongozwa na Wakoloni waliowahi kutawala katika Bara la Afrika
hawapendi kuona Nchi za Afrika zinapiga hatua za Maendeleo kwa wananchi
wake na badala yake hupenda kuripoti na kutangaza mambo mabaya
yanayohusu Afrika ikiwemo njaa, magonjwa, vurugu za kisiasa, vita n.k.
Aidha Dkt. Mwakyembe alisema yapo
mambo mazuri ya Maendeleo yanayofanyika katika Nchi za Bara la Afrika
ikiwemo Tanzania ambayo zimepiga katika kipindi cha miaka minne imepiga
hatua kubwa katika Maendeleo ya kiuchumi, na miundombinu, jambo ambalo
baadhi ya vyombo vya habari vya Mataifa ya Nje ya Afrika yamekuwa
hayapendi kuyatangaza, hivyo ni wajibu wa vyombo vya habari kutumia
majukwaa yao kutetea na kutangaza mafanikio hayo.
“Wakati Hayati Mwalimu Julius
Nyerere na Kenneth Kaunda wa Zambia walipoamua kujenga Reli ya Tazara,
walipingwa vikali sana Wakoloni waliotuwala na wengine waliita reli ile
kuwa ni bamboo (mianzi) lakini ni taifa moja tu la Serikali ya Jamhuri
ya Watu wa China walitusaidia na leo hii reli ile ndiyo ndefu zaidi
katika Bara la Afrika yenye urefu wa kilometa 1860” alisema Dkt.
Mwakyembe.
Kwa mujibu wa Waziri Mwakyembe
alisema Maendeleo ya Bara la Afrika yatatetewa na kupiganiwa na Wafrika
wenyewe, hivyo ni wajibu wa vyombo vya habari vya Bara hilo kujitokeza
na kutetea Maendeleo hayo na kamwe haitatokea siku moja chombo cha
habari cha BBC au CNN vikatangaza mafanikio hayo kwani hawapendi kuona
Mataifa waliyoyatawala yakifikia hatua kubwa za kimaendeleo.
Akifafanua zaidi Dkt. Mwakyembe
aliwataka Vijana wa Nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania kujifunza
historia ya Bara lao ili kuweza kufahamu wapi walipotoka na wapi
wanapoelekea badala ya kupenda kulalamika pasipo na kuweka mikakati ya
namna bora ya kupiga hatua za kujietea Maendeleo yao ya kijamii na
kiuchumi.
Waziri Mwakyembe alisema ni
wajibu wa Taasisi mbalimbali za Habari na Mawasiliano zilizopo katika
Bara la Afrika kujenga mifumo imara ya mawasiliano ikiwemo kutumia vyema
mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuchapisha habari zinazohusu masuala
ya maendeleo badala ya kutumia majukwaa hayo kuandika mambo yasiyo na
faida wala tija kwa mataifa yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, alisema
Serikali imeendelea kuimarisha ushirikiano na taasisi za mawasiliano
katika sekta binafsi ili kuhakikisha kuwa wanajenga daraja moja katika
kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo ya sekta ya habari na Mawasiliano
nchini.
Naye Rais wa Chama cha Maafisa
Uhusiano wa Sekta binafsi Tanzania (PRST) Loth Makuza alisema, taasisi
hiyo ni jukwaa huru linalotoa fursa na nafasi ya kujadili masuala
mbalimbali ya mawasiliano nchini ikiwemo changamoto na utatuzi wa
masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya habari na mawasiliano nchini.
Anaongeza kuwa Taasisi hiyo kwa
kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano imeweza kutengeneza majukwaa
mbalimbali yanayotangaza masuala mbalimbali ya kimaendeleo yaliyofikiwa
katika Nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania, lengo likiwa ni
kubadili mtazamo hasi wa Bara la Afrika katika nyanja za kiuchumi,
kijamii kupitia ngazi ya kimataifa na duniani kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment