Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Prof. Siza Tumbo akiwahutubia wadau wa kilimo alipokutana nao
katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya serna iliyopo Dare s salaam
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Prof. Siza Tumbo akiwahutubia wadau wa kilimo alipokutana nao
katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya serna iliyopo Dare s salaam
Mkuu wa Kitengo cha Mazingira Cha wizara ya kilimo Bi
Shekwanannde Natai akiongea na wadau wa kilimo kutoka sehemu mbalimbali hapa
nchini wakti wa mkutano uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa
Serena uliopo Dar es salaam
Na
Bashiri Salum, Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Prof. Siza Tumbo ameomba wadau wa Kilimo kufadhili mradi wa kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi ili
kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa
yakiathiri kilimo hapa nchini.
Akiongea wakati wa kikao cha
wadau kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena iliyoko
mjini Dar es salaam amesema kwamba mradi huo ni muhimu hasa katika kipindi hiki
ambacho mvua hazitabiriki ambapo utasaidia kubadilisha hali ya kilimo kwa
kuwajengea uwezo wakulima katika maeneo yaliothiriwa zaidi na mabadiliko ya
tabianchi.
Aidha prof. Amesema kwamba
mradi huo unagharimu jumla ya dola za kimarekani milioni 60 ambapo dola milioni
30 zitatolewa na mfuko unaofadhili kilimo (GCF) na dola za kimarekani milioni
30 zinatakiwa kutolewa na serikali au wadau wengine.
“Tumewaita
ili tuweze kujadili namna ambavyo tunaweza kushirikiana nanyi katika kuchangia
kiasi hicho cha dola milioni 30 ili tuweze kuwasaidia watanzania kupitia mradi
huu wa kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabia ya nchi”
,alisema Prof Tumbo
Mkuatno huo ulihudhuriwa na
wadau mbalimbali wakiwemo NEPAD, GCF, SUA FAO DFID ICRAF CARE na International
na wawakilishi wa wizara mbalimbali ambapo walionesha nia ya kuchangia kwa namna
yeyote mradi huo.
Michango ya Kitaifa ya
Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Nationally Determined Contributions) ya
mwaka 2016 iliyowasilishwa kwenye
Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi alimalizia prof.Tumbo.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mazingira
Wizara ya Kilimo Bi Shekwanande Natai
amesema mradi huo ukipata fedha utasaidia wakulima zaidi ya milioni 1.5 katika
mikoa saba (7) ya Tanzania bara na mine
(4) ya Zanzibar
Mikoa itakayofaidika na mradi
huu kwa tanznia bara ni Arusha, Dodoma,Kilimanjaro,Manyara,Singida, Shinyanga
na Tabora na kwa Zanziba ni Unguja Kaskazini,Unguja Kusini Pemba Kaskazini na
Pemba kusini alisistitiza mama Natai.
Awali mama Natai amesema
kwamba mradi utasaidia kujenga uwezo
na kuondoa udhaifu uliopo katika utunzaji aridhi ya kilimo pamoja na uwezo
mdogo wa kukabiliana na athari za tabianchi.
Amesema kwa kupitia mradi huo
wakulima na wafugaji watapa elimu juu ya uapatikanaji wa mitaji na masoko ya
bidhaa zao na sekta biafsi itaweza
kushiriki kikamilifu katika kupambapana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mwongozo wa Kilimo
Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi umeandaliwa kutokana na nyaraka
zinaoonyesha dhamira ya Serikali za kufanya sekta ya kilimo iweze kuhimili
mabadiliko ya tabianchi hadi kufikia mwaka 2030 alimalizia mama Natai.
Elirehema Swali ni moja ya
watafiti ambao wameshughulika na uaandaaji wa maradi wa mradi huo
utashughulikia uongezaji wa thamani
katika mazao ya mafuta kama
alizeti na mazao ya nafaka kama mtama
Alienedelea kusema kwamba
Mahitaji ya Utekelezaji na Uendelezaji wa Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya
Tabianchi yanahusisha uboreshaji uzalishaji na kuongeza tija, kujenga
ustahimilivu wa kukabiliana na mabadiliko
ya tabianchi
Bwana Elirehema Swali
alibainisha kwamba katika wasilisho lake kwamba mradi utasaidia Kuunganisha
mnyororo wa thamani Utafiti kwa ajili ya maendeleo ya kilimo na Kuimarisha na
kuendeleza huduma za ushauri wa kilimo pamoja na Utabiri wa hali ya hewa.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment