Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Vyombo Vya Habari Mbadala (Alternative Media), wakinasa matukio jana jijini Dodoma wakati Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan akihitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi hao kuhusu sheria mbalimbali za habari ili kutekeleza kwa weledi mradi wa Utetezi na Ushawishi kwa kutumia Takwimu (Data Driven Advocacy-DDA), unaosimamiwa na UTPC kupitia Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) kwa ufadhili wa taasisi ya Freedom House.
Picha na Kadama Malunde, Malunde 1 Blog
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan akizungumza kwenye kwenye kilele cha mafunzo ya siku mbili kuanzia Mei 21-22, 2019 kwa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Altenative Media) yaliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan aliwahimiza waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kuhakikisha mategemeo ya mradi huo wa utetezi na ushawishi kwa kutumia takwimu yanatimia.
Wakili James Marenga ambaye alikuwa Mkufunzi wa Mafunzo hayo akitoa salamu zake.
Afisa Program kutoka UTPC, Victor Maleko akitoa ufafanuzi kwenye kilele cha mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) kupitia mradi wa utetezi na ushawishi kwa kutumia takwimu (DDA), Midraji Ibrahim akitoa salamu zake kwenye kilele cha mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Arusha Press Club, Claude Gwandu akitoa salamu zake kwenye hitimisho la mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada kutoka kwa Wakili James Marenga.
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Na George Binagi
Muungano wa
Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), umekamilisha taratibu za
kulichukua Shirikisho la Klabu za Waandishi wa Habari katika nchi za Afrika na
Karibiani (African and Caribbean Press Club-ACP) ambapo makao makuu yake
yatakuwa jijini Dodoma.
Mkurugenzi
wa UTPC, Abubakar Karsan aliyasema hayo jana wakati akihitimisha mafunzo ya
sheria mbalimbali za habari kwa waandishi wa habari wa Vyombo vya Habari Mbadala
(Alternative Media) yaliyofanyika Morena Hoteli jijini Dodoma kwa siku mbili
kuanzia Mei 21, 2019.
“Waambieni
watanzania jambo hilo, waambieni watu wasioijua UTPC jambo hilo, waambieni watu
wenye mashaka na UTPC jambo hilo, kwamba sasa tunaisimamia “Federation” (shirikisho)
ya nchi zaidi ya 160” alisema Karsan akisisitiza kwamba hilo si jambo dogo bali
ni hatua kubwa.
Aidha Karsan
alitumia nafasi hiyo kushukru uwepo wa mradi wa DDA ambapo alisisitiza
washiriki wake kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kuhakikisha matarajio
yanafikiwa na kuondokana na changamoto ya kutotimiza makubaliano jambo ambalo
limekuwa likisababisha taasisi nyingi ikiwemo za waandishi wa habari kuvunjika.
Naye
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari (APC), Claude Gwandu alisisitiza
kwamba klabu hiyo itahakikisha mradi huo unafanikiwa na kwamba haitasita
kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayetaka kukwamisha mradi huo lengo likiwa ni
kuleta mabadiliko katika jamii na taifa kwa ujumla.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative
Media) kupitia mradi wa utetezi na ushawishi wa haki za binadamu kwa kutumia
takwimu (DDA), Midraji Ibrahim alisema mafunzo hayo yatawasaidia kupiga hatua katika
majukumu yao ikiwa kila mmoja atafanyia kazi yale aliyojifunza huku akiishukru
taasisi ya Freedom House kwa ushirikiano wake.
Mradi wa
Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) unafadhiliwa
na Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House
pamoja na PACT kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka jana 2018 ambapo kwa
waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media)
unasimamiwa na UTPC kupitia APC.
0 comments:
Post a Comment