Mwakilishi wa Watengenezaji
mifuko mbadala kutoka katika Kampuni ya Kutengeneza Mifuko Mbadala ya
Gin Investement limited, Mr. Daniel, akizungumza na Waandishi wa
habari(hawapo pichani) kuhusu uzalishaji wa Mifuko mbadala leo Jumatano
22 Mei 2019, Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Watengenezaji
mifuko mbadala kutoka katika Kampuni ya Kutengeneza Mifuko Mbadala ya
Mifuko Enterprises, Irfan Khakhi, akizungumza na Waandishi wa
habari(hawapo pichani) kuhusu uzalishaji wa Mifuko mbadala, leo Jumatano
22 Mei 2019, Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Watengenezaji
mifuko mbadala, Sarah Pima, akizungumza na Waandishi wa habari(hawapo
pichani) kuhusu uzalishaji wa Mifuko mbadala, leo Jumatano 22 Mei 2019,
Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwakilishi wa Watengenezaji mifuko
mbadala Allen Kimambo.
…………………………………………………………
UMOJA wa Wazalishaji wa Mifuko
Mbadala Nchini imewaondoa hofu Watanzania na kusema kuwa vipo viwanda
vya kutosha vya kuzalisha mifuko hiyo hapa nchini na hivyo kuweza
kutosheleza mahitaji ya soko ya bidhaa hiyo ifikapo Juni Mosi, mwaka
huu.
Akizungumza na waandishi wa
vyombo vya habari leo Jumatano (Mei 22, 2019) Jijini Dar es Salaam
kuhusu Mipango na Mikakati ya Umoja huo katika uzalishaji wa mifuko
mbadala nchini, Mwakilishi wa Umoja huo Allan Ngumbuke alisema
Watanzania hawana budi kubadili mtazamo kuhusu matumizi ya mifuko ya
plastiki inayoisha matumizi yake Mei 31, mwaka huu.
Aliongeza kuwa mara baada ya
Serikali kutoa Tamko kuhusu Katazo la Mifuko ya plastiki ifikapo Mei 31,
mwaka huu na kuanza kutumika kwa mifuko mbadala kuanzia Juni Mosi,
mwaka huu Umoja huo walijipanga kikamilifu kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu na mafunzo mbalimbali, ili kuwafanya
Watanzania kuona kuwa mifuko mbadala ni sehemu ya kujiongezea kipato.
“Baada ya katazo la matumizi ya
mifuko ya plastiki, wazalishaji wa mifuko mbadala wameongeza kasi ya
uzalishaji na wengi wameshaagiza mashine zipo njiani kuja na nyingine
zinatengeneza mifuko mbadala, mfano hai ni Tanpak Tissue Paper Ltd,
Hanpal, Green Earth Paper Products Ltd, Harsho Group” alisema Ngumbuke.
Kwa mujibu wa Ngumbike alisema
uzalishaji wa mifuko mbadala utaibua viwanda vingi vya nyumbani, kwani
teknolojia yake ni rahisi na pia mifuko hiyo inayozingatia utunzaji wa
mazingira ipo ya aina nyingi na itakuwepo ya kutosha kuendana na
mahitaji ya soko na ukuaji wa uchumi na hivyo kuendelea kuhudumia soko
la ndani na nje ya nchi.
Aidha Ngumbuke aliwataka wadau na
wananchi wanaotaka kuwekeza kwenye mifuko mbadala kuwa zipo malighafi
za kutosha zinayopatikana katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo kwa
malighafi ya karatasi inayopatikana katika viwanda vya Mufindi Paper
Mills Ltd na Tanpak Tissue Ltd wakati kwa upande wa malighafi ya
vitambaa laini zitapatikana katika cha kiwanda cha Harsho Group
kilichopo Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
“Tunaiomba Shirika la Viwanda
Vidogovidogo Nchini (SIDO) waweke kipaumbele na viatamizi vya uzalishaji
wa mifuko mbadala kwa kuwa SIDO ipo nchi nzima na ni mahiri kwa kutoa
mafunzo ili washiriki wake wataleta matokeo chanya na makubwa kwa haraka
zaidi” alisema Ngumbuke.
Kwa upande wake Afisa Tawala wa
Kiwanda cha Tanpak Tissue Ltd, Michael Mjungu alisema kiwanda chake
kimejipanga kikamilifu kuzalisha malighafi za kutosha kwa ajili ya
uzalishaji wa mifuko hiyo na kuwataka wafanyabiashara kuondoa hofu
kuhusu uwezo wa viwanda vya ndani ya Tanzania kuweza kuzalisha mifuko
mbadala.

0 comments:
Post a Comment