Na Mwandishi Wetu.
TIMU ya Stand United ya Shinyanga, maarufu kama Chama la Wana’ leo
imeipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuchapwa
mabao 2-0 na JKT Tanzania 2-0 Uwanja wa Meja Isamuhyo, Mbweni mjini Dar
es Salaam.
Mabao yaliyoizamisha Stand United leo yamefungwa na washambuliaji wa JKT
Tanzania, Samuel Kamuntu dakika ya 51 na Najim Magulu dakika ya 73.
JKT Tanzania iliyorejea msimu huu Ligi Kuu, imenusurika kushuka baada ya
kumaliza na pointi 47 katika nafasi ya 10, wakati Stand United
imemaliza nafasi ya 19 kwa pointi zake 44, ikiungana na African Lyon
kuteremka daraja.
Nazo Kagera Sugar ya Bukoba na Mwadui FC ya Shinyanga zitamenyana na
timu za Daraja la Kwanza, Pamba SC na geita Gold kuwania kubaki Ligi Kuu
katika mechi za mchujo.
Hiyo ni baada ya Kagera Sugar inayofundishwa na Nahodha wa zamani wa
timu ya taifa ya Tanzania, Mecky Mexime kulazimishwa sare ya 1-1 na Mbao
FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza na Stand United kushinda 3-1
dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Kagera Sugar imemaliza nafasi ya 18 kwa pointi zake 44 sawa na Mwadui iliyomaliza ya 17 kwa wastani nafuu wa mabao.
MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA LIGI KUU LEO
Coastal Union 0-0 Singida United.
Mbeya City 0-0 Biashara United.
Mtibwa Sugar 0-0 Simba SC.
Ruvu Shooting 1-0 Alliance FC (Fully Zullu Maganga 25’ p) . .
JKT Tanzania 2-0 Stand United (Samweli Kamuntu 51’, Najimu Maguli 73’).
Ndanda SC 1-3 Mwadui FC (Kigi Makasi : Ottu Joseph 39’, 41’, Salim Aiyee 61’) .
Yanga SC 0-2 Azam FC (Daniel Amoah 45’+2, Mudathir Yahya 50’).
Mbao FC 1-1 Kagera Sugar (Hebert Lukindo 60’ : Ally Ramadhan 20’).
Tanzania Prisons 3-1 Lipuli FC (Benjamini Asukile 29’, Adam Adam 48’, 85’ : Seif Rashid 46’).
African Lyon 0-2 KMC FC (Cliff Buyoya 21’, 17’)
0 comments:
Post a Comment