Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiwasilikiza wadau wa
Sekta ya Afya kutoka nchini Poland kwenye kikao cha kujadili masuala
mbalimbali yanayouhusiana na Afya na jinsi Nchi hiyo inavyoweza kusaidia
kuimarisha na kuboresha Sekta ya Afya nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Mhe. Selemani Jafo akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ALVO
MEDICAL nchini Poland Bw. Tadeus Olszewski ambaye anaeezea dhumuni la
kuwekeza katika sekta ya afya nchini kwenye kikao cha kujadili masuala
mbalimbali yanayouhusiana na Afya na jinsi Nchi hiyo inavyoweza kusaidia
kuimarisha na kuboresha Sekta ya Afya nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akipokea kitabu cha wasifu
wa nchi ya Poland kwenye kikao cha kujadili masuala mbalimbali
yanayouhusiana na Afya na jinsi Nchi hiyo inavyoweza kusaidia kuimarisha
na kuboresha Sekta ya Afya nchini.
………………
Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameishukuru Serikali ya
Poland kwa kuonyesha nia ya dhati ya kuisadia Tanzania katika Sekta ya
Afya Nchini ili kuboresha na kupunguza changamoto katika Sekta hiyo.
Mhe. Jafo ameyasema hayo wakati wa kikao
na wadau wa maendeleo katika Sekta ya Afya kutoka Poland cha kujadili
masuala mbalimbali yanayouhusiana na Afya na jinsi Nchi hiyo inavyoweza
kusaidia kuimarisha na kuboresha Sekta ya Afya nchini.
Mhe. Jafo ameishukuru Serikali ya Poland
kwa ushirikiano wanatoa katika Miradi mbalimbali ya maendeleo na
kutambua umuhimu wa sekta ya afya nchini kwa kuwa bila kuimarisha Sekta
ya afya hakutakuwa na maendeleo na kushindwa kufikia uchumi wa kati.
“Sekta ya afya ni muhimu kwa jamii, jamii
isipokuwa na afya bora hakutakuwa na maendeleo, hivyo ni vyema Serikali
ikajikita kuwekeza katika Sekta ya afya kwa kuhakikisha inajenga
miundombinu bora, uwepo wa vifaa na vifaa tiba ili kuboresha huduma za
afya nchini” Amesema Mhe. Jafo
Amesema kuwa hatuwezi kufikia uchumi wa
kati endapo watu wetu hawatakuwa na afya bora, ili watu wafanyekazi kwa
bidi waweze kuzalisha na kulipa kodi inavyotakiwa wanatakiwa kuwa na
afya bora hivyo tunawakaribisha wadau mbalimbali wa Sekta ya afya
kuwekeza katika Sekta hiyo.
Mhe. Jafo amendelea kuishukuru Serikali
ya Poland kwa kuonyesha nia ya kuisaidia Serikali mkopo wenye gharama
nafuu utakaosaidia kuimarisha na kuboresha sekta ya Afya nchini lengo
likiwa ni kupunguza changamoto mbalimbali katika sekta hiyo.
Ameiomba Serikali ya Poland kujikita
zaidi katika kusaidia kwenye kuimarisha huduma za msingi hasa ujenzi wa
Vituo vya afya na upatikanaji wa vifaa na vifaa tiba kwa kuwa ndipo
kwenye changamoto kubwa katika suala zima la utoaji wa huduma na
itasaidia kupunguza vifo kwa jamii
Mhe. Jafo amefafanua kuwa katika eneo la
Sekta ya Afya Serikali itapata fursa ya kusaidiwa ujenzi wa Vituo vya
afya, ambavyo vitakuwa vya mfano kwa kuwa na vifaa vyake na kuwa na
nyumba zaidi ya nne za madaktari na hivyo kupunguza changamoto zilizopo.
Mhe. Jafo amelishukuru shirika la Light
For Africa kwa kuunganisha nchi ya Poland na Tanzania ambao
wameonyesha nia ya dhati katika kusaidia masuala ya Sekta ya Afya nchini
jambo ambalo litasaidia kuleta maendeleo kwa jamii
Aidha Wadau hao watatembelea, Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hospitali ya Mirembe,
Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Hospitali ya Amana na Hospitali ya Wilaya
ya Kisarawe kwa lengo la kuangalia ni namna Tanzania inavyotoa huduma
za afya na kuangalia maeneo ambayo wanaweza kusaidia katika kutumia
fursa walizonazo.
0 comments:
Post a Comment