Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira
Mgalu,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kijiji
cha Chibwegere kwa ajili ya kuwasha umeme upande wa kulia ni Mkuu wa
wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mhe.Jabir
Shekimweri akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chibwegere wakati wa
hafla ya kuwasha umeme ambapo Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu
amekata utepe wa kuwasha umeme.
Meneja wa Wilaya ya Mpwapwa Beatus
Kabwe,akisoma taarifa kwa mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Nishati
Mhe.Subira Mgalu (hayupo pichani) wakati alipofanya ziara ya kuwasha
umeme katika kijiji cha Chibwegere.
Mbunge wa jimbo la Kibakwe George
Simbachawene,akizungumza na wanachi wa kijiji cha Chibwegere kabla ya
kumkaribisha Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu ambaye alifanya
ziara ya kuwasha umeme katika kijiji hicho
Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira
Mgalu,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chibwegere alipokuwa
amefanya ziara ya kuwasha umeme kulia kwake ni Mbunge wa jimbo la
Kibakwe George Simbachawene na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa
Jabir Shekimweri.
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha
Chibwegere wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira
Mgalu (hayupo pichani) leo alipofanya ziara ya kuwasha umeme katika
kijiji hicho.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira
Mgalu,akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika kijiji
cha Chibwegere wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma leo Mei 24,2019.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi
pamoja na wananchi wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Nishati
Mhe.Subira Mgalu (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuwasha umeme
katika kijiji cha Chibwegere wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma leo Mei
24,2019.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira
Mgalu,akiwaonesha wananchi kifaa cha umeme (UMETA) wakati wa hafla ya
kuwasha umeme katika kijiji cha Chibwegere wilaya ya Mpwapwa mkoani
Dodoma leo Mei 24,2019.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira
Mgalu,akikata utepe kwa ajili ya uzinduzi wa kuwasha umeme katika kijiji
cha Chibwegere wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma leo Mei 24,2019.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu
akiwasha umeme katika kijiji cha Chibwegere wilayani Mpwapwa Mkoani
Dodoma alipofanya ziara leo Mei 24,2019.
Picha na Alex Mathias-Wazo hurublgo
……………………
Na.Alex Mathias,Mpwapwa
Ikumbukwe kuwa Mei 7,2019 WAZIRI wa
Nishati, Dk.Medard Kaleman aliagiza kukamatwa na kutiwa mbaloni kwa
Mkandarasi wa kampuni ya OK Electrical Contractor aliyekuwa akisambaza
umeme wa mradi wa REA awamu ya III katika wilaya ya Mpwapwa kutokana na
kutokamilisha kuwasha umeme katika kijiji cha Chibwegere
Hatimaye leo Mei 24,2019 Naibu Waziri wa
Nishati Mhe.Subira Mgalu amefanya ziara ya kuwasha umeme katika kijiji
cha Chibwegere wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma ikiwa ni juhudi za
Serikali za kuhakikisha kila mwananchi aweze kuunganishiwa umeme.
Mhe.Mgalu akizungumza
na wananchi huku akitoa elimu kuhusu gharama za kuwaunganishia umeme
amesema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli inawajibu ya
kuwajali na kuwathamini wananchi wa kipato cha chini.
Amesema kuwa Serikali imeamua kushusha gharama za kuwaunganishia umeme wananchi wake hadi shilingi 27,000/= tu.
“Hapo mwanzo gharama za
kuunganishiwa umeme zilikuwa ni shilingi 177,000, lakini Serikali kwa
vile inawajali wananchi wake imelipa shilingi 150,000/= kwa kila
anayeweka umeme, na kazi ya mwananchi ni kulipia kiasi kidogo tu cha
shilingi 27,000/=, tofauti na hapo awali.” amesema Mhe.Mgalu
Aidha amesema kuwa wapo
wananchi wanaoishi karibu na miundombinu ya njia ya umeme na sio kwamba
wanashindwa kulipa shilingi elfu 27,000/= bali wanashindwa na gharama
ya kutandaza umeme ndani ya nyumba (wiring) inayofanywa na
wakandarasi.(mafundi).
“Gharama hizo za wiring zimeonekana kuwa ndio changamoto kwa wananchi na
serikali imepokea changamoto hizo na kuwa itazifanyia kazi.”
amesisitiza
Naibu Waziri huyo ameutaka uongozi wa
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Dodoma na Mpwapwa
kuhakikisha wanakamilisha usambazaji wa umeme kwa wanakijiji ili waweze
kunufaika na huduma hiyo.
Aidha Mhe.Mgalu amefafanua kuwa lengo la
Serikali ni kuhakikisha wanafikisha huduma ya umeme kwa wananchi ambapo
hadi kufikia Desemba mwaka huu watakuwa wamekamilisha kazi hiyo ya
kusambaza umeme vijijini nchi nzima na kubakiza kazi ya kuwaunganishia
wananchi
Naye Mbunge wa jimbo la Kibakwe George
Simbachawene, ameishukuru serikali kwa kazi kubwa wanayofanya ya
kuwasambazia wananchi umeme na kusema kuwa maendeleo yanakua kwa kasi
kubwa inayotokana na kasi ya Rais, Dk.John Magufuli ya kuwajali wananchi
hasa wenye hali ya chini.
Alimuomba Naibu waziri kuwapelekea umeme
wananchi wa kijiji cha Msisili ambacho kipo jirani na Chibwegele ili nao
waweze kupata huduma hiyo.
Jimbo la Kibakwe mpaka sasa vijiji 42
tayari vimeshapata umeme huku vikibaki vijiji vinane ambavyo bado
havijapata umeme huku Serikali ikiendelea kusimamia na kuhakikisha kuwa
hadi Disemba vitakuwa tayari vimeshapata umeme
0 comments:
Post a Comment