Mkurugenzi wa Michezo Yusuph
Singo, akizungmza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), leo Jumamosi,
25 Mei 2019, kuhusu Kutoa kibali kwa Makampuni matatu yatakayosafirisha
watanzania kwenda kuiunga mkono Timu ya Taifa (Taifa Stars) katika
Michuano ya Mataifa ya Africa (AFCON) Nchini Misri June 21, 2019 hadi
Julai 19, 2019, kulia kwake ni Mwakilisha wa kampuni ya Clouds Media
Group (CMG), Shafii Dauda na Mwakilishi kutoka World Link, Zaki Admani
Mwakilisha wa kutoka kampuni ya
Clouds Media Group, Shafii Dauda akieleza jambo kuhusu namna ya
kuwasafirisha watanzania watakajitokeza kwenda kuiunga mkono Timu ya
Taifa (Taifa Stars) katika Michuano ya Mataifa ya Africa (AFCON) Nchini
Misri June 21, 2019 hadi Julai 19, 2019, baada CMG kupata kibali hicho
kutoka kwa Serikali, Kushoto ni Mwakalishi kutoka Kampuni ya Travel
Link, Ephrem Mtuya, Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Singo na Mwakilishi
kutoka World Link, Zaki Admani
Mwakilishi kutoka World Link,
Zaki Admani akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),
kuhusu namna ya kuwasafirisha watanzania watakajitokeza kwenda kuiunga
mkono Timu ya Taifa (Taifa Stars) katika Michuano ya Mataifa ya Africa
(AFCON) Nchini Misri June 21, 2019 hadi Julai 19, 2019, Baada ya Kampuni
hiyo kupata kibali hicho kutoka kwa Serikali, Kushoto ni Mkurugenzi wa
Michezo Yusuph Singo
Mwakalishi kutoka Kampuni ya
Travel Link, Ephrem Mtuya, akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari
(hawapo pichani), kuhusu namna ya kuwasafirisha watanzania
watakajitokeza kwenda kuiunga mkono Timu ya Taifa (Taifa Stars) katika
Michuano ya Mataifa ya Africa (AFCON) Nchini Misri June 21, 2019 hadi
Julai 19, 2019, Baada ya Kampuni hiyo kupata kibali hicho kutoka kwa
Serikali Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu kutoka Travel Link, Doreen Gafoor na
kulia ni Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo.
(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)
………………………………………………………………….
MAELEZO-DAR ES SALAAM
SERIKALI kwa kushirikiana na
Shirikisho la Soka Nchini (TFF) imeyataja Makampuni matatu
yatakayotumika kusafirisha Mashabiki wa Soka na Watanzania kwa ajili ya
kuishangilia Timu ya Soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wakati wa
Michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON)
zitakazofanyika Mwezi Juni, mwaka huu nchini Misri.
Akizungumza na Waandishi wa
Vyombo ya Habari leo Jumamosi (Mei 25, 2019), Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Michezo, Yusuph Singo aliyataja Makampuni hayo kuwa ni pamoja na Clouds
Entertainment Group Ltd, Travel Link na World Link, ambayo yalishinda
mchakato wa ushindani na makampuni mengine kutokana na kukidhi vigezo
mbalimbali vilivyoanishwa.
Kwa mujibu wa Singo alisema
Serikali na kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Nchini (TFF) waliamua
kusimamia mchakato wa kupata makampuni hayo ili kuzuia aina yoyote ya
utapeli kwa Watanzania hususani Mashabiki wa Soka wa hapa nchini
watakaojitokeza kwenda Nchini Misri kuipa nguvu ya ushingiliaji Taifa
Stars.
“Katika miaka ya nyuma kulikuwa
na utapeli katika haya makampuni ya usafirishaji, hivyo Serikali kwa
kushirikiana na TFF tumeyapata Makampuni matatu, bei zao zitakuwa rahisi
na wamepanga kuwa na nembo ya pamoja ambayo wataitangaza ili iweze
kujulikana na Watanzania” alisema Singo.
Aidha Singo alisema kuhusu
utaratibu wa visa za kusafiri makampuni hayo kwa kushirikana na TFF
yatatoa taarifa ya jinsi Mashabiki wa Soka watavyoweza kupata huduma
hiyo kabla ya kuanza kwa michuano hiyo inayotarajia kuanza kutimua vumbi
tarehe 21 Juni mwaka huu.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa
Kampuni ya Clouds Entertainment Group Ltd, Shaffih Dauda alisema Kampuni
yao imejipanga vyema kuhakikisha kuwa inatoa huduma zote muhimu kwa
Watanzania watakaosafiri kwenda Nchini Misiri kuishangalia Taifa Stars
ikiwemo visa, usafiri wa ndani, malazi katika kipindi cha siku 10 za
mechi tatu za makundi itayocheza Taifa Stars.
“Clouds Entertainment Ltd kila
mwaka tuna msimu wa kulevya wa soka, mwaka jana tulikuwa na Msimu wa
kulevya wa Kombe la Dunia kule nchini Urusi, na sasa tunarudi Afrika na
tutawahudumia vyema mashabiki watakaojitokeza kwa kiasi cha Dola za
Kimarekani 1650 na pia tutaoa ofa ya Mashabiki hao kutembelea vivutio
mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini Misri” alisema Dauda.
Aliongeza kuwa katika kutoa
urahisi wa huduma kwa Watanzania hususani suala la malazi, Kampuni yao
tayari kwa kushirikiana na wakala wao aliyopo nchini Misri, wamepata
mmoja wa Mitaa maarufu nchini Misri ujulikanao Kilimanjaro ambapo
utawezesha Mashabiki wa Watanzania kupata huduma zote muhimu kuwafanya
Mashabiki hao huko kujiona kuwa wapo nyumbani.
Kwa upande wake, Meneja Maendeleo
ya Masoko wa Kampuni ya World Link, Zaki Admani alisema kampuni hiyo
itatoza kiasi cha Dola za Kimarekani 1550 kwa Mashabiki wa Soka, ambayo
watasafiri kuelekea Nchini Misri pamoja na kutoa ofa ya kuchagua mechi
moja yoyote ambayo mshabiki wa Soka atapenda kuingalia katika timu
zitakazochuana na Taifa Stars.
Aliongeza kuwa kuanzia Jumatatu
ya wiki ijayo Kampuni hiyo itatoa kifurushi kitakachomwezesha Shabiki wa
Soka hapa nchini kuweza kuchagua idadi ya mechi ambazo atapenda
kuziangalia wakati akiwa na Timu ya Taifa Stars nchini Misri.
“Wapo wengine watapenda kuangalia
mechi moja, na hili tumeliangalia na mapema wiki ijayo kuanzia jumatatu
tutatoa utaratibu wake wa namna ya kuwasaidia mashabiki wa aina hii”
alisema Admani.
Naye Meneja Utawala wa Kampuni ya
Travel Link, Ephrem Mtuya alisema kuwa kwa miaka 15 sasa Kampuni hiyo
imekuwa ikifanya kazi pamoja na TFF kwa ajili ya kuwasifirisha wachezaji
wa Timu ya Taifa ya Tanzania katika nchini mbalimbali na hivyo
amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kusafiri na Kampuni hiyo ili
kwenda kuipa nguvu Timu ya Taifa ya Tanzania ikiwa nchini Misri.
Alisema Kampuni imeweka kiwango
cha Dola za Kimarekani 1300 pekee kwa Mtanzania yotote atayapenda
kusafiri na Timu hiyo hususani Mashabiki wa Soka ikihusisha Gharama za
Tiketi ya Ndege, usafiri, pamoja na huduma za malazi.
0 comments:
Post a Comment