Na Mwandishi Wetu
Hatua za serikali kuhakikisha Watanzania wananufaika na
rasilimali za nchi yao na kuongeza mapato zimeanza kuzaa matunda licha
ya kupingwa vikali hapo awali.
Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar-es-Salaam,
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.
Hassan Abbasi, amesema hatua zilizochukuliwa kwenye sekta ya madini na
kuboresha mifumo ya kukusanya mapato ya serikali imechangia kuongeza
mapato maradufu.
Akieleza hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano,
Dkt. Abbasi amesema ni pamoja na ujenzi wa ukuta kwenye eneo la migodi
ya madini ya Tanzanite Mirerani, kuanzishwa kwa masoko ya madini kwenye
mikoa na wilaya nchi nzima na kuundwa kwa mifumo ya kisasa ya kijiditali
ya kurekodi mapato ambayo licha ya kuongeza mapato, lakini pia
imeongeza ufanisi.
Dkt. Abbasi amesema kuwa hadi kufikia mwezi Mei 2019 sekta ya
madini kwa kipindi cha miezi kumi na moja ya mwaka wa fedha 2018/19
mapato yamefikia Shilingi bilioni 302.63 kiasi ambacho ni zaidi ya
mapato yote kiasi cha Shilingi bilioni 301.6 yaliyopatikana kwenye mwaka
wa fedha 2017/18.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Dkt. Abbasi mapato kwenye
sekta ya madini katika kipindi cha miaka minne yamekuwa yakiongezeka
mfululizo, akitolea mfano amesema mwaka 2016/17 makusanyo ya maduhuli
yalikuwa bilioni 214.5 wakati mwaka 2015/16 maduhuli yalikuwa Shilingi
Bilioni 210 na mapatao ya mwaka 2017/18 yalikuwa Shilingi bilioni 301.6
Aidha, aliongeza kuwa mapato yanayotokana na mauzo ya madini ya
Tanzanite tangu ujenzi wa ukuta wa Mirerani ujengwe kuzunguka migodi ya
madini hayo mapato yameongezeka maradufu kutoka kiasi cha shilingi
milioni 71.8 mwaka 2015 hadi kufikia bilioni 1.43 mwaka 2017.
Akieleza mafanikio yaliyopatikana kutokana na uboreshaji wa
mifumo ya kukusanya mapato Dkt. Abbasi amesema mifumo hiyo sio tu
imeongeza mapato, lakini pia imeongeza ufanisi.
“Kabla ya Mfumo wa TTMS Serikali ilikuwa haipati kitu kabisa
katika miito ya simu za nje wala kuwa na uwezo wa kuhakiki mapato ya
simu za ndani lakini tangu mfumo huo ulipofungwa kwa eneo la mapato ya
simu za nje tu Serikali imekwisha kusanya Shilingi bilioni 97.16 ikiwa
ni malipo ya kodi zitokanazo na mapato ya kampuni za simu kwa simu
kimataifa zinazoingia na kuishia hapa nchini” alifafanua Dkt. Abbasi.
Kuhusu ziara ya Rais Magufuli kwenye nchi za Afrika Kusini,
Namibia na Zimbabwe Dkt. Abbasi ameeleza ziara hiyo licha ya kuwa na
lengo la kuimarisha ushirikiano wa kihistoria, lakini pia ilikuwa na
lengo la kutafuta fursa za kibiashara. “Kwenye ziara hiyo Rais Magufuli
ameweza kufikia makubaliano ya kuongeza kiwango cha biashara na
uwekezaji kwenye sekta ya utalii, usafiri wa anga na miundombinu pia
Tanzania imeweza kupata soko la mahindi tani 700,000 nchini Zimbabwe”.
Aidha, Dkt. Abbasi amewasihi Watanzania wenye ujuzi wa
kufundisha Lugha ya Kiswahili kuitumia vyema fursa ya kufundisha lugha
hiyo nchini Afrika Kusini kwa kujisajili kwenye kanzi data ya wataalamu
wa Kiswahili Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ili wapate ithibati
na kutambulika rasmi.
Kuhusu ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, Msemaji Mkuu wa Serikali
amewahakikishia Watanzania majadiliano juu ya mrad huo bado yanaendelea
na Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha maslahi ya nchi yanawekwa
mbele ili wanufaike na rasilimali za nchi yao.
Mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali na vyombo vya habari
umelenga kueleza utekelezaji wa serikali katika sekta mbalimbali ikiwemo
madini, miundombinu, mawsiliano na sekta nyingine.
Thursday, May 30, 2019
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya kilim...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Timu ya Sevilla FC leo wamefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Timu ya...
-
Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungan...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati ya ushauri ya kitaifa kuhusu ute...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment