Mkuu
wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizunguza na wafanyabiashara wa bidha za kusindika walikuwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda
Vidogo (SIDO) Iringa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali
Wafanyabiashara wa bidha za kusindika wakiwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda
Vidogo (SIDO) Iringa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali na wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa bidhaa za kusindika
NA FREDY MGUNDA, IRINGA
Wafanyabiashara wa wilaya
ya Iringa wametakiwa kufanya biashara wakiwa wamelipa kodi au wanatakiwa kuwa
na kitambulisho cha wafanyabishara wadogo wadogo maarufu kama kitambulisho cha
machinga.
Akizungumza na
wajasiliamali waliokuwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda
Vidogo (SIDO) Iringa,mkuu
wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema ni marufuku kwa sasa kufanya
biashara yoyote wilaya ya Iringa bila kulipa kodi na zile ambazo hazijafikia
hatua kodi zitalipa tozo
“Sasa tunaanza kufanya
mchakato wa kuchunguza kujua wafanyabiashara wangapi wanafanya kazi hizo bila
kulipa kodi na tutawachukulia hatua kwa mujibu wa sheria za nchi zinavyosema”
alisema Kasesela
Kasesela aliwataka
wafanyabiashara wadogowadogo wote wa wilaya ya Iringa kuhakikisha wanapata
kitambulisho cha kwa shilling elfu ishirini ambacho kinatamruhusu kufanya
biashara sehemu yoyote hapa nchini kwa mujibu wa Rais
“Jamani ili ufanye
biashara kwa uhuru katika wilaya ya Iringa ni lazima uwe na kitambusho cha
wafanyabisahara wadogo au uwe umelipia leseni kutoka katika mamlaka husika la
sivyo huwezi kufanya biashara hiyo wilaya ya Iringa” alisema Kasesela
Kasesela aliwataka
wananchi wote wanaopenda kufanya biashara kuhakikisha wanafanyabiashara kwa
kufuata taratibu zilizowekwa na nchi ili wasipate usumbufu wowote ule kutoka
kwa mamlaka za wilaya ya Iringa.
“Jamani wananchi wa Iringa
changamkieni kuchukua vitambulisho vya wafanyabishara wadogo wadogo ili kufanya
biashara zenu mkiwa na uhuru wa kutosha ila mkikahidi mkono wa sheria utawahusu”
alisema Kasesela
Aidha Kasesela aliwashauri
wafanyabishara ya bidhaa za kusindika kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa
kufuata kanuni za kisheria kwa kuhakikisha wanalipa kodi kama inavyostahili.
Nao baadhi ya
wafanyabiashara wadogo wadogo walimuadi mkuu wa wilaya hiyo kuwa
watahamasishana kuhakikisha wote wanakuwa na vitambulisho hivyo ili wafanye
biashara kwa uhuru na haki.
“Mkuu tunakuhakikishia
kuwa tutafanyabiashara huku tukiwa tumevaa vitambulisho hivi kwa kuwa Rais wetu
katupa uhuru wa kufanya biashara zetu mahali popote pale bora mradi tuwe na
vitambulisho hivyo” walisema wafanyabiashara hao
0 comments:
Post a Comment