Mkurugenzi wa Utawala na Fedha kutoka BRELA, Bw. Bakari Mketu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake kutembelea wafanyabiasara na kutoa elimu juu ya masuala ya usajili, ikiwemo matumizi ya mfumo mpya wa usaji kwa njia ya mtandao(Online Registration System-ORS)..Mjini Bariadi Simiyu.
Bi. Suzan Senso kutoka BRELA(kulia) akimsikiliza Bi .Neema Joseph Meneja wa Kituo cha Mafuta cha JBS Mjini Bariadi wakati wa ziara yake na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha kutoka BRELA, Bw. Bakari Mketu kwa wafanyabishara iliyolenga kutoa elimu juu ya masuaa ya usajili ikiwemo matumizi ya mfumo mpya wa usaji kwa njia ya mtandao(Online Registration System-ORS).
Na Stella Kalinga, Simiyu
Wafanyabiashara hapa nchini
wametakiwa kusajili biashara zao kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni
(BRELA) ili ziweze kutambuliwa kirahisi na waweze kufanya biashara
kwa ushindani wa Kitaifa na Kimataifa.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya
wafanyabiashara Mjini Bariadi Mkoani Simiyu mara baada ya kutembelewa na
Maafisa kutoka BRELA katika maeneo yao ya biashara kwa lengo la kufuatilia
masuala mbalimbali ya Wakala huo ikiwa ni pamoja kutoa elimu na kuangalia
mwitikio wa mfumo wa usajili wa biashara kupitia mtandao (Online Registration
System-ORS).
“ Kuna faida sana kwa mfanyabiashara
kusajili biashara yake BRELA kwanza inatambulika, usajili pia utamsaidia kupata
urahisi hasa kwa makampuni yanayotaka kuingia mkataba na yeye, akihitaji huduma
za kifedha katika benki na utamsaidia kutangaza biashara yake popote”
“Kampuni yoyote inayotaka kuingia
mkataba na sisi ni lazima inaomba nyaraka za usajili wa BRELLA, tukitaka huduma
za kifedha kwenye benki nao wanahitaji nyaraka za BRELA, yapo manufaa makubwa
kusajili BRELA” Lucy Sabu Mkurugenzi Msaidizi, Hoteli ya Sweet Dream Bariadi.
Naye Bi Neema Joseph Meneja wa Kituo
cha mafuta JBS Bariadi ameshukuru BRELA kwa kuanzisha usajili wa biashara
kupitia mtandao(Online Registration System-ORS) jambo ambalo amesema
litawawasaidia wafanyabiasha kufanya usajili mahali walipo badala ya kusafiri
kufuata huduma hiyo Dar es salaam kama ilivyokuwa awali.
Aidha, Bi. Neema ameomba BRELA
iendelee kutoa elimu kuhusu umuhimu wa usajili wa biashara kwa wafanyabiashara
na matumizi ya mfumo mpya wa usajili kupitia mtandao ili uweze kufahamika
vizuri zaidi kwa wafanyabiashara.
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha kutoka
BRELA, Bw. Bakari Mketu amesema mara baada ya kutoa elimu ya usajili miezi
miwili iliyopita kiwango cha usajili kimeongezeka na kufikia asilimia 80 ya
lengo walilojiwekea kwa robo zote tatu ndani ya mwaka .
“Tumesajili kampuni 4678 zaidi
ya 66% huku malengo yakiwa kusajili 7110 na kusajili majina ya biashara
8022 zaidi ya 49% huku malengo yakiwa kusajili majina 1640 kwa robo
zote tatu .... kwanza tulikuwa tunapanda taratibu ...tutaendelea
kuwaelimisha wateja wetu ili kuhakikisha wateja wote wanakuwa uelewa wa
kutosha.
Katika hatua nyingine Mketu ametoa
rai kwa wanasheria kuzingatia sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwa
ni pamoja na masuala yanayohusiana na Usajili, ili kuepuka usumbufu kwa
wafanyabiashara.
‘’Sheria ni taaluma ambayo bado
inaheshimika sana, kujifunza kila siku ndio taaluma inavyotaka sisi hatuwezi
kuwafundisha kazi…lakini tunaomba wazingatie sheria wakati wakifanya majukumu
yao, mathalani kuna mwanasheria alifanya zoezi la kubadili hisa za mteja (share
transfer) pasipo kufuata utaratibu ambao umeainishwa kisheria na TRA”
alisema Mketu.
Naye Suzana Senso kutoka BRELA
amesema ni vema Wanasheria wanapofanya kazi kujiridhisha kwanza juu ya taratibu
na sheria zinazotakiwa kufuatwa katika kazi husika ili waweze kuwasadia wateja
wao kwa kuzingatia sheria na taratibu.
“Naomba nitoe rai kwa wanasheria,
ukipata kazi uliza wengine taratibu zilivyo ili uweze kumsaidia
mteja, huyu mama alitaka kuhamisha hisa (share transfer) mwanasheria akaja
akachomoa nyaraka na kuweka nyingine akamweleza kuwa utaratibu umekamilika
wakati utaratibu ulipaswa ufanyike TRA; kutokana na uelewa wa mama na
afisa biashara mkoa wao walitutafuta, najiuliza ni wangapi wanakutana na
changamoto hizi” alihoji Bi. Suzan Senso.
Aidha, Bi. Elizabeth Samweli kutoka
Kampuni ya Mlashi General Supplies alikiri kukumbwa na changamoto hiyo ya
mwanasheria kufanya zoezi la kuhamisha hisa pasipo kufuata
utaratibu uliowekwa kisheria na kushukuru BRELLA kwa namna walivyomsaidia mara
baada ya kuwaeleza changamoto hiyo; huku akisisitiza BRELA kuendelea kutoa
elimu.
Maafisa kutoka Wakala wa Usajili wa
Biashara na Leseni (BRELA) wako Mjini Bariadi Simiyu kwa ajili ya kuendelea
kutoa elimu juu ya usajili wa biashara kwa wafanyabiashara mkoani hapa pamoja
na wajasiriamali walio katika Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Waadventista
Wasabato(ATAPE) ambao unafanyika Mkoani Simiyu.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment